Ubashiri Mechi ya Inter Milan Vs AC Milan Jumanne Hii

[Picha: sportco.io]

Mwanadishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Ukiwa ni Usiku wa derby Della Madonnina ambao utashuhudia Inter-milan watakapo kichapa dhidi ya AC-Milan katika nusu fainali za mzunguko wa pili wa Coppa Italia.

Uwanja wa Giuseppe Meazza ali-maarufu Kama San Siro unaomilikiwa na manispaa ya Milan ndio utatumika pia katika mzunguko huu wa pili wa nusu faili katika mechi hiyo ya Ac Milani dhidi ya Inter Milan.

Katika mechi hii Inter Milan wao wako Katika Hali nzuri ya wachezaji kwani hawana majeruhi Wala mchezaji anayeweza kukosa mechi hii.

Soma pia: Tetesi za Lewandowski kuhamia Barcelona

Lakini kwa upande wa Ac Milan wao wanacheza wakiwa hawana wachezaji wao Kama Simon Kjær, Alessandro Florenzi, Alessio Romagnoli, Matteo Gabbia pamoja na Zlatan Ibrahimovic.

Inter Milan dhidi ya Ac Milan siyo Mara yao ya kwanza kukutana na wala haiwezi kuwa Mara yao ya mwisho kwani katika mechi tano za nyuma walizokutana Inter Milani wao wameshinda mechi 2 Huku wao Ac Milan wakishinda mechi 1 na droo imetokea katika mechi 2.

Free Download: Pakua mixes 7 Kali za Clouds FM ndani ya Mdundo

katika msimamo wa Ligi kuu Seria A Timu hizi mbili ndizo vinara katika ligi hiyo ambapo Ac Milan wao ndio wanaoshika nafasi ya kwanza kwa kuwa na alama 71 huku inter Milan wakiwa Nafasi ya pili kwa alama 69

Baada ya mechi hii mshindi ataenda kukutana na mshindi wa nusu fainal ya Juventus na Firontina baada ya mechi yao kuchezea Jumatano hii.

Kwenye mechi ya moto Kama hii na katika Hali ya kuwa ni mzunguko wa mwisho wa nusu fainali kwa timu zote mbili, odds zilizowewa kwa timu zote mbili kufunga ni 1.82

Leave your comment