Tetesi za Lewandowski kuhamia Barcelona

[Picha: express.co.uk]

Mwanadishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Mara baada ya kudumu katika misimu nane ya Bundesliga Sasa tetesi zilizopo mitandaoni  zinasema kuwa mshambuliaji Robert Lewandowski straika Makini kabisa tokea Bayern Munich ya Ujerumani anauwezekano wa kuhamia La liga huko Uhispania.

Lewandowski mwenye umri wa miaka 33 kwa Sasa anaripotiwa kutaka kuingia mkataba na Barcelona ambao wameonesha Nia ya dhabiti kabisa katika kusaka saini ya straika huyo ambapo Lewandowski inasemekana amekuwa na shauku kubwa ya kujiunga na Barcelona au Real Madrid katika maisha yake ya soka.

Download FREE DJ Mixes on Mdundo.com

Akiwa ni mchezaji muhimu sana kwa Bayern ambapo tangu ajiunge na Timu hiyo kutokea Borussia Dortmund mwaka 2014 mpaka sasa Bayern Munich ndio mabingwa wa Ligi hiyo ya Ujerumani huku akiwa ameifanikisha timu hiyo kupata UEFA Champions , UEFA Super Cup, FIFA Club World Cup pamoja na German Supercup.

Mpaka Sasa inasemekana kuwa Bayern Munich wanawezakana kuhitaji kiasi cha Euro milioni 70 mpaka Euro milioni 80 ili Barcelona waweze kumpata  mshindi huyo wa tuzo za FIFA kwa mwaka 2021, huku wao Barca wakidaiwa kuweka mezani dau la Euro milioni 30 kutokana na umri wa mchezaji huyo.

Kwa Sasa Barcelona katika kukamilisha safu ya ufungaji imesajili wachezaji kama Pierre-Emerick Aubameyang aliyetoka Arsenal,Ferran Torres kutoka  Manchester City pamoja na Adama Traore aliyechukuliwa kwa mkopo kutokea Wolverhampton Wanderers.

Lewandowski kwa Sasa ndiye mchezaji anayeongoza kwa magoli huko Champions league licha ya kuwa usiku wa Jana timu yake ilitolewa na Villarreal katika hatua ya robo fainali za Champions league.

Pia Lewandowski mpaka Sasa katika ligi ya Bundesliga msimu wa mwaka 2021-2022 amefanikiwa kuifungia timu yake ya Bayern magoli 32 katika mechi 29 alizocheza mpaka sasa, hii inaonesha ni jinsi gani straika huyu anavyoweza kuisaidia Barcelona ambapo mkataba wake unasemekana kuisha mwishoni mwa majira ya joto mwakani

 

Leave your comment