Wasifu wa Goodluck Gozbert , Nyimbo Zake Bora, Tuzo Alizoshinda, Mahusiano na Thamani Yake

[Picha: Music in Africa]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Goodluck Gozbert ni nani?

Jina: Goodluck Gozbert

Tarehe ya Kuzaliwa: Aprili 12, 1991

Aina ya mziki: Mziki wa Injili

Thamani ya jumla: Haijulikani kwa sasa

Soma Pia: Nyimbo za Injili za Kiswahili Kwenye Mdundo (Pakua bila Malipo)

Goodluck Gozbert ni mwimbaji wa nyimbo za injili  kutoka Tanzania. Goodluck anajulikana kwa sauti yake nyororo. Goodluck alizaliwa Mwanza na kwa sasa anaishi Dar es Salaam.

Fungu la Leo Zaburi 118:14

Goodluck Gozbert  alianza Muziki  vipi?

Tangia utotoni mwake Goodluck Gozbert alikuwa na hamu ya kuimba na kufanya mziki. Katika mahojiano ya hapo awali, Gozbert alisema kuwa hakuwa na nia ya kufuata muziki kama taaluma lakini kwa sababu ya ugumu wa maisha alilazimika kukuza talanta yake. Alijitolea kama mtayarishaji jijini Mwanza kitu ambacho kilimpa msingi wa kazi yake. Mwanzo, Gozbert alijulikana kama Lollipop wakati alikuwa tu mwandishi wa muziki.

Soma Pia: Rose Muhando Vs Christina Shusho: Nani Msani Bora wa Nyimbo za Injili?

Wakati wa kazi yake ya uandishi wa muziki, alifanya kazi na wasanii wakubwa kama vile Ben Pol na Ommy Dimpoz. Muziki wake unapata msukumo kutokana na uzoefu wake wa maisha. Hivi sasa, Gozbert anatengeneza muziki chini ya lebo yake ya kurekodi .

Nyimbo maarufu za Goodluck Gozbert?

  • Simu
  • Hasara Roho
  • Umeshinda Yesu
  • Kama si yeye
  • Ipo siku
  • Shukrani Nibaliishe
  • Mama
  • Mwenye Majibu
  • Pendo Langu
  • Shukurani

Soma Pia: Nyimbo Mpya za Injili 2021 [Video]

 Goodluck Gozbert ameshinda Tuzo ngapi?

Katika kipindi chake katika muziki,Gozbert aliteuliwa na kushinda tuzo kadhaa katika ukanda wa Afrika Mashariki. Mnamo mwaka wa 2019, alipokea mataji tano wakati wa Tuzo za Maranatha Afrika Mashariki ambazo zinaheshimu matendo bora ya injili kutoka Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda, Burundi, Sudan Kusini, Ethiopia, Eritrea, na Somalia

Mnamo mwaka wa 2015, Goodluck Gozbert alishinda Msanii wa Kiume wa Mwaka wa Afrika Mashariki kwenye Tuzo za Sauti, na Msanii Bora wa Injili / Wimbo wa Mwaka kwenye Tuzo za Xtreem. Katika mwaka huo huo, alishinda pia Msanii Bora wa Nyimbo za Injili Tanzania / Wimbo wa Mwaka kwenye Tuzo la Xtreem.

Soma Pia: Pakua Mixtape 5 Bora za Nyimbo za Injili

Goodluck Gozbert ana thamani gani?

Goodluck Gozbert hajatangaza thamani yake ya mali na hela anazomiliki. Ila ni mojawapo wa wasanii wanaopata pesa zao kwa kuuza mziki wao kwa njia zozote zikiwemo za mfumo wa kidijitali.

Goodluck Gozbert yuko kwenye uhusiano?

Goodluck Gozbert kwa sasa bado hajaoa na haijulikani kama ana mahusiano na mtu yeyote. Hivi sasa, hakuna habari ya taarifa inayopatikana kuhusu hali yake ya uhusiano.

Leave your comment