Nyimbo Mpya za Injili 2021 [Video]

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Jiunge Nasi Kwenye Telegram

Mziki wa Injili nchini Tanzania unaendelea kupata umaarufu zaidi na mwaka huu wa 2021, wasanii wa injili hawakusazwa katika uachia nyimbo mpya za injili.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Christina Shusho Aachia Video Mpya ‘Hesabu’

Katika nakala hii, tunaangazi nyimbo hizo mpya za mwaka huu:

Usipigane - Joel Lwaga

Usipigane ni wimbo unaomaanisha vita ni vya Bwana. Kwenye wimbo, Joel anatuarifu kuwa unapopigana, Mungu huenda kupumzika na unapopumzika Yeye (Mungu) huenda anakupigania. Joel Lwaga aliachia wimbo huu wiki mbili zilizopita na kufikia sasa amapata watazamaji zaidi ya elfu sabini na nane kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=qNIHhBzk5u0

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Ngoma 5 Zinazotamba Mdundo Tanzania [Video]

Hesabu - Christina Shusho

Kwa sauti yake ya kupendeza, Shusho aliachia wimbo huu hivi karibuni na anatuambia jinsi alivyofanya hesabu zake na kuona kuwa ni Mungu tu aliyemtendea miujiza. ‘Hesabu’ ni kazi yake ya pili Christina tangia mwaka uanze huku akitarajiwa kuachia nyimbo zaidi mwaka huu.

https://www.youtube.com/watch?v=he5DFZPs6jY

Mugambo – Goodluck Gozbert ft Bonny Mwaitege

Msanii wa muziki wa injili nchini Tanzania Goodluck Gozbert aliungana na staa nguli wa muziki Boni Mwaitege kwa wimbo mpya unaitwa 'Mugambo'. ‘Mugambo’ inahimiza watu kusonga mbele bila woga. Kufikia sasa wimbo huu una watazamaji zaidi ya milioni moja.

https://www.youtube.com/watch?v=ZRa5zuUKMT8

Sitalia- Irene Robert ft Christina Shusho

Huu ni wimbo wa ushirikiano kutoka kwa wasanii Irene Robert na Christina Shusho ambapo wanaapa kutolia tena ila watamuamini Mungu katika maisha magumu wanayopitia. Irene Robert ni msanii wa injili kutoka Tanzania anayekua kwa kasi na wimbo huu unaendelea kupokelewa na mashabiki.

https://www.youtube.com/watch?v=MTpKgyhk8aw

Karibu Home - Bamboo ft Martha Mwaipaja

‘Karibu Home’ ni wimbo wa kwanza kutoka kwa Bamboo African Bantu kutoka Kenya ambapo amemshirikisha mwimbaji maarufu toka Tanzania Martha Mwaipaja. Huu ni wimbo ambao unaangazia hadithi ya Mwana mpotevu. ‘Karibu Home’ ni kazi ya Bamboo ya kwanza baada ya muda mrefu.

 https://www.youtube.com/watch?v=6NfthlLN4f8

Leave your comment