Nyimbo Mpya: Christina Shusho Aachia Video Mpya ‘Hesabu’

[Picha: Christina Shusho Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Tumia Rafiki Kwenye WhatsApp

Mwanamuziki was ngoma za injili nchini Tanzania Christina Shusho ameachia wimbo mpya wa kusisimua kwa jina 'Hesabu'.

Kwa sauti yake ya kupendeza, Shusho anatuambia jinsi alivyofanya hesabu zake na kuona kuwa ni Mungu tu aliyemtendea miujiza.

Soma Pia: Diamond Atamba Kwenye Orodha ya Nyimbo Kumi Bora Mdundo Tanzania

‘Hesabu’ ni kazi yake ya pili Christina tangia mwaka uanze huku akitarajiwa kuachia nyimbo zaidi mwaka huu.

Kwa jumla, wimbo huu unazungumzia namna Mungu tu ndio kigezo cha usalama wetu hapa duniani. Anabainisha nyakati ngumu za maisha na hata nyakati alizokuwa na furaha yote ikiwa kwa uwezo wake Mungu.

“Nimehesabu, Nakuhesabu Nimehesabu, Nakuhesabu Nimeongeza na kutoa Nikazidisha na kugawanya, Nimeona ni wewe, Yesu ni wewe tu, Hakuna mwingine, Yesu ni wewe tu…” anaimba Christina katika wimbo huu wa kusisimua.

Soma Pia: Rayvanny Aachia ‘Number One' Remix Akimshirikisha Enisa

Video ya wimbo huu inaangazia watu wanaofanya vibarua vidogo vidogo ili kujikimu. Hili likiwa onyesho kuwa Mungu ndiye mpaji wa kila siku hivyo ni himizo kwa watu kuamini kuwa mwenyezi Mungu ndiye anasaidia katika hesabu zote za maisha.

Shusho anazidi kuonyesha ufundi wake katika mziki wa injili nchini Tanzania huku wanamziki wengi wakiazimia kufanya ushirikiano naye.

Kanda hii imeandaliwa na kutengezwa na director Hascana wa Tanzania. Kwa upande mwingine, wimbo huu umepokelewa vizuri na mashabiki na nambari za watazamaji zinaendelea kuongezeka.

https://www.youtube.com/watch?v=he5DFZPs6jY

Leave your comment