Nyimbo Mpya: Rayvanny Aachia ‘Number One' Remix Akimshirikisha Enisa

[Picha: WCB na Enisa Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Tumia Rafiki Kwenye WhatsApp

Msanii kutoka lebo ya Wasafi Rayvanny ameachia wimbo mpya kwa jina ‘Number One Remix’.

Hii ni video ya pili kutoka kwa albamu yake ya “Sound From Africa”. Rayvanny amemshirikisha binti muamerika Bi Enisa Nikaj.

Read Also: Nyimbo Tano za Rayvanny Zilizompa Umaarufu Bongo

Enisa anatambulika kwa kazi zake nzuri kama vile ‘Love Cycle’ iliotamba sana mwaka jana kwenye mtandao wa TikTok.

‘Number One Remix’ imetengezwa kwa ujuzi mkubwa ikizingatiwa ni uridio wa wimbo wake Rayvannyy na Zuchu.

Enisa alifanya wimbo huu mjini New York kwa sababu ya janga la korona.

Read Also: Nyimbo Mpya: Diamond Atamba Kwenye Orodha ya Nyimbo Kumi Bora Mdundo Tanzania

Wimbo huu unaangazia mada tofauti za mapenzi, kama kuthamini na kuwa pamoja kwa kila mmoja.

Mistari ya mapenzi inawekwa katika vitendo na wanamuziki hawa wawili wanapomuimba mwenzao na kujieleza mbona yeye ni ‘Number One’.

Huku Rayvanny akiendelea kudhihirisha ufundi wake katika mziki wake, Enisa kwa sasa amepata fursa ya kujitambulisha katia soko la Afrika Mashariki.

Video hii ilitengezwa na director Eris Mzava wa Extra Focus production inayokisiwa kuwa kampuni mpya ya Rayvanny.

Kufikia sasa, wimbo huu umepokelewa kwa kishindo huku ikiwa na watazamaji zaidi ya elfu themanini masaa chache baada ya kuzinduliwa.

https://www.youtube.com/watch?v=MbRkyXd4ohA

Leave your comment