Nyimbo Mpya: Ngoma 5 Zinazotamba Mdundo Tanzania [Video]
2 March 2021
[Picha: Grammy]
Mwandishi: Omondi Otieno
Mwezi wa Februari umekua wenye shamrashamra na mbwe mbwe yenye maudhui ya mapenzi.
Wasanii wengi kutoka Bongo waliachia mziki unaoambatana dhana hii, huku wasanii wengine kama Diamond Platnumz wakiendelea kuvuna matunda ya ngoma zao walizoachaia kitambo, lakini bado zafanya vyema.
Katika nakala hii, tunaangazia ngoma tano zinazovuma mwezi huu moya wa Machi 2021, na zile unazoweza kupakua bure kwenye mtandao wa Mdundo.
Hii hapa orodha hio:
Waah - Diamond akimshirikisha Koffi Olomide
‘Waah’ no mojawapo ya nyimbo zake Diamond zilizo na utazamaji mwingi zaidi katika mda mfupi. Licha ya wimbo huo kuachiwa mwaka uliopita, bado unavuma Tanzania. Kumshirikisha Koffi kwenye wimbo huu umeusaidia kufikia watu wengine kwani wasanii wote wan wafuasi wengi dunia nzima.
Soma Pia: Nyimbo Mpya: Collabo 5 Zake Diamond Zinazovuma Bongo [Video]
Mama Amina - Marioo
Kwenye wimbo huu, Marioo amewashirikisha Sho Madjozi wa Afrika Kusini na Bontle Smith.
‘Mama Amina’ ni wimbo wa kupendeza ambapo Marioo anafurahishwa na msichana fulani anayemwita 'Mama Amina'. Wimbo huu ni mojawapo ya nyimb zinazoskizwa sana Bongo na unaweza kuipat bure kuisikiliza na kuipakua bure kwenye mtandao wa Mdundo.
Wapo - Harmonize
Wimbo huu wa Harmonize ulizua tetesi huku wengi wakisema kuwa aliutumia kumsuta msanii tajika Diamond Platnumz.
Kwenye wimbo huu, Harmonize anaangazia watu wasioridhika na kile walichanacho.
‘Wapo’ ni wimbo uliopokelewa vizuri na unavuma Bongo hadi sasa. Wimbo huu uko kwenye mtandao wa Mdundo na unaweza kupata bure.
Soma Pia: Nyimbo Mpya: Video Kumi Bora Tanzania Februari 2021
Number One - Nandy
Kwenye wimbo huu, Nandy amemshirikisha msani tajika kutoka Nigeria Joeboy. ‘Number One’ ni wimbo wa mapenzi ambapo wasanii hao wawili wanaeleza jinsi wanavyowapenda na kuwadhamini wapenzi wao. ‘Number One’ ndio kazi yao ya kwanza pamoja na ilipokelewa vyema. Wimbo huu uko kwenye Mdundo na unaweza kuupakua bure.
Loyalty - Darassa
‘Loyalty’ ni mojawapo ya nyimbo kutoka kwa album mpya ya Darassa kwa jina ‘Slave Becomes A King’. Kwenye wimbo huu, amewashirikisha wasanii tajika kutoka Tanzania; Nandy na Marioo. ‘Loyalty’ ni wimbo unaongazia umuhimu wa kuwa kuaminifu kwenye sekta ya mapenzi.
Hizi tano ni baadhi tuu ya ngoma zinazofanya vyema kwenye mtandao wa Mdundo Tanzania. Ili kupata nyimbo nyingine mingi, tafadhali tembelea kurasa hii: https://mdundo.com/tz
Leave your comment