Nyimbo Mpya: Collabo 5 Zake Diamond Zinazovuma Bongo [Video]

[Picha: Diamond Platnumz Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Jiunge na Channel ya Mdundo Telegram

Msanii shupavu Diamond Platnumz anajulikana kama kigezo kikubwa katika fani ya mziki wa Bongo. Hivyo ushirikano wake na wasanii wengine huwa kama baraka kwao anapowapa motisha katika ukuaji wa mziki wao.

Katika nakala hii, tunaangazia nyimbo tano ambzao Diamond ameshirikisha wasanii wengine au kuhirikishwa nao.

Waaaaah – Diamond na Koffi Olomide

Diamond Platnumz aliachia wimbo huu akimshirikisha nguli wa mziki wa Congo Koffi Olomide.Video ya ‘Waah’ ni mchanganyiko ngoma kutoka kizazi cha Koffi Olomide na kizazi cha Diamond. Kufikia sasa ni wimbo ulio na watazamaji zaidi ya millioni arobaini na nane.

https://www.youtube.com/watch?v=HCuTwNgY3_M

Shusha - Babalevo na Diamond

Wimbo huu ulikua wa dhamira ya kuonyesha ubabe wao katika mziki .Huu ulikua ushirikano wa Babalevo na Diamond Platnumz uliompa Babalevo nafasi ya kupata watazamaji wengi ambao ni zaidi ya milioni mbili.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Rayvanny Aachia ‘Number One' Remix Akimshirikisha Enisa

https://www.youtube.com/watch?v=ph1UQR1etYQ

Bado Sana - Lava Lava na Diamond

Wimbo huo ulitolewa siku chache kabla ya mwaka mpya na kwa sasa ni moja ya nyimbo kubwa nchini Tanzania. 'Bado Sana' inaangazia watu ambao wanadhani wameshahitimu maishani, lakini jamii ina dhana nyingine kuwahusu. Kwenye YouTube, 'Bado Sana' inafanya vizuri sana na zaidi ya watazamaji milioni 4.

https://www.youtube.com/watch?v=QN7o76eulRs

Far Away – Lava Lava na Diamond

Ni wimbo kutoka EP ya Lava Lava ya ‘Promise’. Far away ni wimbo unaongazia uzuri wa wapenzi walio na ukaribu sana. Kufikia sasa ni wimbo uliopata usikilizaji mkubwa kwenye mtandao wa YouTube na Watazamaji zaidi ya laki nane.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Video Kumi Bora Tanzania Februari 2021

https://www.youtube.com/watch?v=5JP6Ikdu-K4

Cheche - Zuchu na Diamond

Huu ulikua ushirikiano wa kwanza wake Zuchu na Diamond Platnumz ambapo kufikia sasa ndio wimbo mkubwa zaidi kutoka kwake Zuchu na watazamaji zaidi ya milioni kumi na saba.

https://www.youtube.com/watch?v=vyUslddxOpI

Leave your comment