Zuchu vs Nandy: Ni nani Bora Zaidi?

[Picha:Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Nandy na Zuchu ni wasanii tajika kutoka Bongo na kwa sasa ndio wanaosifika zaidi kutoka kanda ya Afrika Mashariki. Hivi karibuni Nandy na Zuchu wamelinganishwa sana na mashabiki kila mmoja kutaja msanii wake kama aliye bora zaidi nchini Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla.

Hivyo katika nakala hii tunaangazia uwezo wa kina dada hawa wawili katika sanaa:

Uzoefu

Nandy ni msanii anayesifika kwa tajriba ya kuwa kwenye mziki rasmi kwa miaka mitano sasa. Zuchu kwa upande wake ana mwaka mmoja tu katika tasnia ya muziki. Kwa hili, mara mingi Zuchu ameonekana kumuheshimisha Nandy kama msanii jambo ambalo liliwafanya mashabiki wengi kumpa hongera. Zuchu anatumaini kufanya kazi na Nandy kwa wakati utakaofaa.

Soma Pia:  Tembo Vs Chui: Harmonize, Rayvanny Waachia Nyimbo Mpya ‘Vibaya’ na ‘Nyamaza’

Tuzo

Nandy ana Tuzo zaidi ya Zuchu kwa kuwa alianza muziki miaka kadhaa kabla ya Zuchu. Katika Tuzo za Afrimma mwaka 2020 Nandy alishinda Tuzo ya msanii bora wa Kike Africa Mashariki huku Zuchu akituzwa  msanii chipukizi wa huo. Tuzo zingine za Nandy ni kama vile; Msanii Bora wa Kike Africa Mashariki mwaka wa 2017 (All Africa Music Awards), Msanii Mpya wa Kike (AMI Awards Afrika) mwaka wa 2018 na zingine mingi.

Pakua Nyimbo Zake Nandy Bila Malipo Kwenye Mdundo

Albamu

Kufikia sasa Zuchu hajaachia albamu ila ana EP kwa jina “I am Zuchu” ambayo ilikua yake ya kujitokeza kama msanii. Kufikia sasa ana nyimbo kumi na nne na zingine za ushirikiano. Kwingineko Nandy ana albamu mbili “The African Princess”2018 na “Wanibariki” EP 2021 na nyimbo nyinginezo za ushirikiano.

Soma Pia: Wasifu wa Zuchu, Nyimbo Zake Bora, Tuzo Alizoshinda, Mahusiano na Thamani Yake

 Usajili na Utazamaji kwenye mtandao wa YouTube

Nandy anashabikiwa kama msanii wa pili wa kike Afrika mashariki mwenye watazamaji zaidi ya milioni mia moja na usajili wa mashabiki zaidi ya laki saba. Zuchu ndani ya mwaka mmoja ameweka rekodi mbali mbali na nyimbo zake. Kufikia sasa, Zuchu ndio msanii wa kwanza wa kike kutoka Afrika mashariki aliye na watazamaji zaidi ya milioni mia moja arobaini na nane na ana wasajili zaidi milioni moja kwenye chaneli yake ya YouTube.

Soma Pia: Mafanikio 5 Kuu ya Zuchu Mwaka Mmoja Baada ya Kuzinduliwa na WCB

Wafuasi Kwenye Instagram

Kwenye mtandao wa Instagram, Nandy ana wafuasi milioni nne nukata nane ilhali Zuchu ana wafuasi milioni bili nukta tano. Mtandao wa Instagram ni muhimu kwenye tasnia ya muziki kwani inasaidia wasanii kusambaza kazi zao mpya. Pia, ni rahisi kupata biashara kutoka kwa kampuni kubwa kubwa iwapo una wafuasi wengi kwenye Instagram.

Leave your comment