Tembo Vs Chui: Harmonize, Rayvanny Waachia Nyimbo Mpya ‘Vibaya’ na ‘Nyamaza’

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Wasanii wakubwa wa Bongo Harmonize na Rayvanny walianza wiki hii kwa upande mbaya. Wawili hao ambao sasa wanaonekana mahasidi wa mziki , wameachia ngoma mbili zinazogusia ugomvi wao wa mahusiano na familia ya muigizaji Kajala na mwanawe Paula.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Ngoma Tano Kali Kutoka Konde Music Worldwide Mwaka 2021

Kwa upande wake Harmonize , ameachia wimbo kwa jina “Vibaya”. Katika wimbo huu anaangazia uhusiano wake wa awali na wapenzi wake. Katika ushairi wake, Harmonize anatumaini kutosemana vibaya na akina dada hao.

Kwingineko, Rayvanny kwa upande wake anatupa michambo kwa wimbo mpya kwa jina ‘Nyamaza’.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Diamond, Mbosso Waachia Video ya Ngoma Yao 'Baikoko'

Wimbo huu unamlenga Tembo kwa tuhuma za kujihusisha na mama na pia kumtaka mwanawe.

"Pigo za kusema vya ndani mi sinaga hizo ama kumtafuta mchawi mi nani kuongezea tatizo Tulia hapa tutakuwa wa ndani hadi Paradiso, na tukatangaza kweiupe mambo ya hadharani na tattoo ndizo hizo," aliimba Harmonize.

https://www.youtube.com/watch?v=zEtsp8BlyM4

Rayvanny naye anasema ni Bora Tembo angenyamaza au aombe radhi ya tuhuma hizo alizopata. Katika “Nyamaza” Rayvanny anamkumbusha Tembo alivyojaribu kumchochea ili akamatwe kwa kuwa katika uhusiano na binti wa Kajala ambaye ni Paula.

“Nivizuri #kunyamaza maana inayoumia ni familia ambayo ina ndugu jamaa na wazazi na wanaumia pia,,, unapofanya kosa ni vizuri kuomba radhi huo ndio uungwana lakini pia kila anaekufanyia roho mbaya kwa chuki na uadui mwambie ajue chuki hazijengi bora kunyamaza…” aliimba Rayvanny.

https://www.youtube.com/watch?v=FRhxiyDhoyw

Wakati kiki ya Rayvanny na Harmonize inaendelea nyimbo hizi mbili “Vibaya” na “Nyamaza” zimepokelewa vizuri na mashabiki na zina watazamaji zaidi ya laki tatu na zaidi ya laki moja mtawalia.

Leave your comment