Nyimbo Mpya: Ngoma Tano Kali Kutoka Konde Music Worldwide Mwaka 2021

[Picha: Konde Music Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Lebo ya msanii Harmonize Konde Music Worldwide ni mojawapo ya lebo yenye umaarufu sana nchini Tanzania. Lebo hio imekua kwenye kipaumbele katika kuachia ngoma zinazovuma nchini humo.

Soma Pia: Rais Samia Suluhu Ashauri Serikali yake Kuzingatia Changamato za Wasanii

katika nakala hii, tunaangazia nyimbo tano kali kutoka lebo hiyo mwaka huu wa 2021:

Anajikosha - Harmonize

‘Anajikosha’ ni wimbo unaoangazia wahusika wenye hulka potovu. Kimsingi Harmonize anawachambua watu wenye tabia ya kujigamba kwa vichache walivyonavyo. Wimbo huu unabeba mdundo wa Amapiano ambao unatambaa Afrika kwa sasa.

https://www.youtube.com/watch?v=Qv7z9jpjMwk

Kama Anjella ft Harmonize

Huu ni wimbo wa kwanza kutoka kwa msanii Anjella baada ya juinga rasmi na Konde Gang. ‘Kama’ ni wimbo unaoangazia mahitaji ya watu wawili wanaotamani kuwa katika uhusiano.

https://www.youtube.com/watch?v=z2LHODzQ1JA

All Night Harmonize ft Anjella

Harmonize aliachia wimbo huu siku ya Wapendanao almaarufu Valentine’s Day. Huu ni wimbo wa mapenzi ambapo Harmonize anamsifia mpenzi wake kwa namna anavyompenda.

https://www.youtube.com/watch?v=D8fmQfzrGgo

Asante Magufuli –Konde Music artists

Wimbo huu uliachiwa kwa ajili ya kumuomboleza aliyekuwa Rasi wa Tanzania marehemu Dkt. John Pombe Magufuli. Wasanii hawa wanamshukuru marehemu Magufuli kwa kupigania maslahi ya wanyonge nchini humo. Kwao wanasema kama nchi walimpenda rais wao ila Mungu kampenda zaidi. Kufikia sasa ni wimbo ulio na watazamaji zaidi ya milioni tatu.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Ibraah Aachia Video Mpya ‘Mapenzi’

https://www.youtube.com/watch?v=CqEvlLonyB8

Mapenzi – Ibraah

Katika wimbo huu Ibraah anaangazia uchungu ulioko ndani ya uhusiano ya mapenzi. Ibraah anasema kuwa katika maisha binadamu anaweza vumilia vitu vingi ila tu si mapenzi.

https://www.youtube.com/watch?v=q_0A3pvSehs

Leave your comment