Rais Samia Suluhu Ashauri Serikali yake Kuzingatia Changamato za Wasanii

[Picha: President Samia Suluhu Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Tanzania inapoendelea kuomboleza kifo cha aliyekuwa rais Dkt. John Pombe Magufuli, chini ya uongozi mpya wa Rais Bi, Samia Suluhu nchi hiyo inaendelea kupata masharti mpya ya kuendeleza matukio yake.

Katika upande wa sanaa na mawasiliano, Rais huyo ametangaza kuwapasapoti wasanii akisema kuwa vijana wanahitaji kupewa nguvu zaidi ili kujikimu kimaisha.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Ibraah Aachia Video Mpya ‘Mapenzi’

“Wasanii na wanamichezo ni ajira, hivyo tukiwapa nguvu na kutatua changamoto zao, vijana wengi wataweza kujiaajiri . Hivyo naomba mkaliangalie hilo kwa mapana," Rais Suluhu Hassan alisema hivi majuzi.

Hayati rais Magufuli alikua kwenye kipaumbele katika kuwahusisha wasanii katika mikakati yake na alisifiwa kwa kuwakutanisha mahasidi wa mziki Alikiba, Diamond Platnumz na Harmonize wakati wa kampeni zake hapo mwaka jana.

Vilevile, Rais Suluhu ameagiza wizara ya Habari, Utamudini, Sanaa na Michezo kuvifungulia vyombo vyote vya habari vilivyofungiwa na kushauri uhakikisho kuwa vyombo hivyo vinafwata sheria na kanuni zilizowekwa kuendesha taratibu za sekta hiyo.

Soma Pia: Rosa Ree Azua Gumzo Baada ya Kuachia Wimbo Mpya ‘Satan’

Kwingineko, Rais Samia ameagiza adhabu ziwe wazi kwamba chombo kikifanya kosa fulani adhabu yake ni fulani, hali itakayosaidia isionekane kuwa Serikali inaminya uhuru wa vyombo vya habari.

”Wizara ya Habari, nasikia kuna Vyombo vya Habari mmevifungia, vifungulieni lakini wafuate sheria na miongozo ya Serikali, tusiwape mdomo wa kusema tunaminya uhuru wa vyombo vya habari, tusifungie tu kibabe” alisema Rais Samia.

Leave your comment