Nyimbo Mpya: Ibraah Aachia Video Mpya ‘Mapenzi’

[Picha: Ibraah Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii toka lebo ya Konde Music Worldwide Ibraah ameachia kanda ya wimbo wake ‘Mapenzi’.

‘Mapenzi’ ni mojawapo ya nyimbo tatu alizoachia kwenye kazi yake ya ‘Karata tatu’ iliyotoka mapema mwakani.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Rayvanny, Juma Jux Waachia Video ya Wimbo Wao ‘Lala’

Katika wimbo huu, Ibraah anaangazia uchungu ulioko ndani ya uhusiano ya mapenzi. Ibraah anasema kuwa katika maisha binadamu anaweza vumilia vitu vingi ila tu si mapenzi.

Anasisitiza kuwa mapenzi huumiza sana. Kwake mapenzi yana wenyewe.

“Amini unayempenda, naye ana wake anayependa pia, Na siku zinakwenda aah, Na hata yule anayempenda, Naye ana wake anayemwita dear, Haya mapenzi mwana kwenda aah…” aliimba Ibraah.

Soma Pia: Rosa Ree Azua Gumzo Baada ya Kuachia Wimbo Mpya ‘Satan’

Kanda hii ina maandhari ya kupendeza kuanzia bustani za starehe na hata pwani za bahari.

Maandalizi ya wimbo yalifanywa na ustadi wa juu haswa kuzingitia kua ni mkato wa picha hizi ulifanya na maigizo ya vituko ambavyo hufanyika katika uhusiano.

Ubunifu ulioko kwenye kanda hii ni wa mwelekezaji Joma kutoka RedShot huku mdundo wa wimbo huu ukiwa wake Mr. Simon.

Kufikia sasa wimbo huu umepokelwa vizuri na mashabiki na katika mtandao wa YouTube “Mapenzi” umefikisha watazamaji zaidi ya elfu themanini.

https://www.youtube.com/watch?v=q_0A3pvSehs&ab_channel=Ibraah

Leave your comment