Rosa Ree Azua Gumzo Baada ya Kuachia Wimbo Mpya ‘Satan’

[Picha: Music in Africa]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii wa Hip-hop kutoka Bongo Rosa Ree amezua gumzo mtandaoni baada ya kuachia ngoma mpya kwa jina ‘Satan’.

Katika wimbo huu, Rosa Ree aliamua kuangazia unyama na ukatili wa mpenzi wake wa kitambo.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Rayvanny, Juma Jux Waachia Video ya Wimbo Wao ‘Lala’

Kwake anamlaumu shetani kwa kumtuma mwanaume huyo kwake kama mpenzi wake ila lengo lake likiwa kumuangamiza.

Anakashifu Shetani kwa kujaribu kumtuma askari wake kama mpenzi wake ambaye alimuonyesha namna ya kutumia dawa za kulevya na vitu vingine vingi.

Hivyo kwa sasa anasema amejificha ndani ya Mungu na yeye tu ndiye anampigania katika maisha.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Nandy Aachia Video Mpya ya Wimbo ‘Wanibariki’

“Satan you sent your soldier to me as my boyfriend, Told him to come and introduce me to that cocaine, I was in love and he said that it was on trend, Now I wonder when the misery is gonna end…” aliimba Rosa Ree.

Wimbo huu lengo lake iliukua kuwahimiza watu wawe waangalifu katika maisha yao. Watambue ni nani watawakaribisha kwao kwani binadamu wengine huwa kama majaribu maishani.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Aslay Aachia Wimbo Mpya 'Vumilia'

Wimbo huu umepokelwa na wengi na hata Rosa Ree mwenyewe amepokea barua kutoka kwa mashabiki wakielezea wanayopitia maishani na vipi wimbo huu umewagusa.

Wimbo huu umeandaliwa na mtayarishaji wa mziki Ibra Jacko na kanda hii ilmeelekezwa na Director Ivan.

Kufikia sasa wimbo huu unaendelea kupata umaarufu na una watazamaji zaidi ya Laki moja.

https://www.youtube.com/watch?app=desktop&v=JkCd5M9AZk0&ab_channel=RosaRee

Leave your comment

Top stories

More News