Nyimbo Mpya: Aslay Aachia Wimbo Mpya 'Vumilia'

[Picha: Music in Africa]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwimbaji maarufu kutoka Tanzania Aslay ameachia wimbo mpya kwa jina ‘Vumilia’.

‘Vumilia’ ni wimbo unaoangazia mwanamume anayempenda mpenzi wake licha ya kuwa na mapato ya chini.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Nandy Aachia Video Mpya ya Wimbo ‘Wanibariki’

Aslay anamuomba mpenzi wake amvumilie kwa kile anachopata wakitumainia maisha mazuri baadae.

Katika mistari ya wimbo huu unapata kuskia ubunifu wake katika fani hii ya RnB ambapo ina utaratibu na uvutio wa upendo.

“Vitu uvitakavyo vizito, Mi kuvipata siwezi, Hali yangu mafuriko,Abariki Mwenyezi, Sitokupa ukitakacho,Kukudanganya siwezi, Nitakupa nilicho nacho,Ndo uwezo wangu mpenzi…”aliimba Aslay.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Video Tano Zinazovuma Wiki Hii YouTube Tanzania

Aslay anasisitizia ahadi za ndoa akimsihi mpenzi wake kumvumilia katika hali zake anapojaribu kutimiza kiapo chake cha ndoa.

Vile vile anaongelea atakavyoumia iwapo mwenzake atamuacha.

Hadi sasa, ‘Vumilia’ imepokelewa vizuri na mashabiki na una watazamaji zaidi ya elfu arobaini kwenye mtandao wa YouTube.

Video ya wimbo huu bado hhaijachiwa, lakini mashabiki wanatumai kwamba itaachiwa hivi karibuni kwa kuwa ‘Vumilia’ ni wimbo mkubwa.

Hii ni wimbo wa tatu Aslay ameachia mwaka huu baada ya ‘Nashangaa’ and ‘Bye Magufuli’.

Wimbo wake wa ‘Bye Magufuli’ ni wenye uchungu mwingi kwani ulikua wa kuomboleza hayati Rais John pombe Magufuli. Wimbo guo una zaidi ya watazamaji elfu mia nane kwenye YouTube.

 https://www.youtube.com/watch?v=cb_d16j2umA

Leave your comment

Top stories

More News