Nyimbo Mpya: Video Tano Zinazovuma Wiki Hii YouTube Tanzania

[Picha: Jambo News]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Licha ya kuwa katika hali ya maombolezo, wasanii wa Tanzania wanaendelea kuachia nyimbo mpya zikiwemo za kumkumbuka marehemu rais John Pombe Magufuli.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Nyimbo 10 Bora Kutoka Bongo Zilizoachiwa Machi 2021 [Video]

Katika nakala hii, tunaangazia nyimbo tano kutoka bongo zinazovuma wiki hii.

Lala Salama - Tanzania All Stars

Wimbo huu umejaa majonzi, simanzi na ufundi kwa pamoja. Wasani zaidi ya ishirini walikuja pamoja kumuaga hayati Magufuli. Katika mtandao wa YouTube ni wimbo unaovuma zaidi licha ya kuwa ni wa huzuni mno.

https://www.youtube.com/watch?v=gD-VdBqHscY&ab_channel=WasafiMedia

Kifo - Rayvanny

Katika wimbo huu Rayvanny anamlilia rais wake akisema ‘Kifo’ hakina huruma. Kufikia sasa ni wimbo uliosikilizwa sana na mashabiki na una watazamaji zaidi ya million Mbili.

https://www.youtube.com/watch?v=McqT-XpgYhQ&ab_channel=Rayvanny

Asante Magufuli – Konde Music

Wasanii wa lebo ya Harmonize waliandaa wimbo wa kumshukuru marehemu Rais Magufuli kwa kupigania maslahi ya wanyonge nchini humo. Kwao wanasema kama nchi walimpenda rais wao ila Mungu kampenda zaidi.Kufikia sasa ni wimbo ulio na watazamaji zaidi ya milioni mbili nukta nane.

https://www.youtube.com/watch?v=CqEvlLonyB8&ab_channel=Harmonize

Yalah - Mbosso

Yalah’ ni wimbo yenye maudhui ya mapenzi kutoka albamu ya Mbosso “Definition of Love…” Kwenye wimbo huu, Mbosso anaeleza kuwa mtu yeyote anaweza kupata mapenzi licha ya kule anakotoka, au kazi anayofanya.

https://www.youtube.com/watch?v=ijm4CHvJdGw&ab_channel=Mbosso

Bye Magufuli - Aslay

Huu ni utungo wake Aslay akiangazia kifo cha Hayati Magufuli. Aslay alijiunga na wasanii wenzake katika kumuomboleza aliyekuwa Rais wa Mungano wa Tanzania. Kufikia sasa ni wimbo ulio na watazamaji zaidi ya ya laki saba kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=IReENAMP8fQ&ab_channel=Aslay

Leave your comment

Top stories