Nyimbo Mpya: Nandy Aachia Video Mpya ya Wimbo ‘Wanibariki’

[Picha: Nandy Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii tajika wa nyimbo za Bongo fleva nandy ameaachia kanda ya wimbo wake mpya wa Injili kwa jina ‘Wanibariki’.

Huu ni wimbo wa kwanza katika EP yake alioachia hivi Karibuni yenye nyimbo tano za kuabudu.

Soma Pia: Pakua Mixtapes Tano Kali za Hip Hop Kutoka Bongo kwenye Mdundo

Katika ‘Wanibarika’, Nandy anaangazia safari yake ya maisha na kumshukuru Mungu kwa baraka alizomjalia.

Anaimba na kusema ni Mungu tu amefanya hatetemeki.

“Ni wewe pekee wanijua vyema kwako siterereki kwame,wanitenda mema na kunipa heshima umenifanya nisimame,na kama nikishikwa na shida ntakimbilia hekaluni mwako,ntaijaza nafsi mbele zako bwana ntasema yote yanayonishinda…”aliimba Nandy.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Ngoma 5 Kali Kutoka WCB Mwaka wa 2021

Katika kanda hii inaonyesha hadithi ya kijana mmoja aliyekuwa na shida na akasaidiwa na mamake Nandy. Baadae maishani mamake Nandy akawa mgonjwa na kwa maajabu yao, daktari aliyemhudumia ni yule kijana waliomsaidia wakati mmoja.

Kwenye video hii, Nandy anaonyesha ubabe wake katika mziki na kusisitiza umuhimu wa kutumia talanta yake kumsifia Mungu wake aliyemjalia hadi alipofika.

Nandy amesema kuwa EP hii ni zawadi kwa masahbiki wake kwa kumkubali katika tasnia ya mziki.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Nyimbo 10 Bora Kutoka Bongo Zilizoachiwa Machi 2021 [Video]

Nyimb zingine kwenye EP yake Nandy ni kama vile; Umenifaa, Asante, Nipo Naye na Noel Song.

Kufikia sasa wimbo huu unaendelea kupata umaarufu kwenye mtandao wa YouTube . Kanda ya wimbo huu ilifanyiwa matayarisho na director Destro wa Wanene Films.

https://www.youtube.com/watch?v=uWhYzj5GU8g&ab_channel=Nandy-TheAfricanPrincess

Leave your comment

Top stories

More News