Nyimbo Mpya: Rayvanny, Juma Jux Waachia Video ya Wimbo Wao ‘Lala’

[Picha: Rayvanny and Jux Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii tajika kutoka Tanzania Rayvanny ameachia kanda ya wimbo wake ‘Lala’ akimshirikisha Juma Jux.

‘Lala’ ni mojawapo wa nyimbo zilizoko kwenye albamu yake ‘Sounds From Africa’.

‘Lala’ ni wimbo ambao wasanii hao waangazia kumzimia binti mmoja ambaye kwenye kanda hii ni mtayarishaji wa video za mziki. Hivyo, Katika harakati za kumfurahisha dada yule, Jux anaimba jinsi anavyoshukuru kuvunjika kwa uhusiano wake wa zamani kwani sasa amepata fursa ya kupenda tena.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Ngoma 5 Kali Kutoka WCB Mwaka wa 2021

“Nawaza usingetokea ningeongea nini leo? (Aah),Bila ya penzi lako ningeenjoy nini leo? (Aah),Imekuwa bora alivyopotea ukatokea wewe leo,Tena bila huruma yako ningetamba wapi leo?” aliimba Jux.

Rayvanny kwa upande wake pia anaonyeshwa kama aliyepagawishwa na binti huyo pia.

Kwingineko, kupitia wimbo huu wawili hao Rayvanny na Juma Jux waliibua gumzo baada ya kuwachamba wapenzi wao wa zamani ambao ni Fayhma almaarufu Fayvanny na Vanessa Mdee mtawalia.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Nyimbo 10 Bora Kutoka Bongo Zilizoachiwa Machi 2021 [Video]

Wasanii hao katika wimbo huu wanasema jinsi wamewasahau, hawaongei na hata kuwablock katika mitandao ya kijamii.

Wimbo huu ulitengezwa kwa ufundi mkubwa kwani ukitazama walitumia mandhari nzuri. Mwelekezaji wa video hii akiwa Hascana.

Video hii imepokelewa vizuri nan i mojawapo ya kazi zinzofanya vizuri Bongo sasa.

https://www.youtube.com/watch?v=s3kdjHUPlXA&ab_channel=Rayvanny

Leave your comment