"Hamna Chochote" Baddest 47 Afunguka Baada ya Kushinda Tuzo


[Picha: Instagram]

Mwandishi-Charles Maganga 

Msanii wa Dancehall kutokea nchini Tanzania, Baddest 47 hivi karibuni ametoa mawazo yake  kufuatia ya kushinda tuzo hivi karibuni kwenye Tanzania Music Awards. 

Kwenye tuzo hizo ambazo zilifanyika Tarehe 29 Aprili mwaka 2023, Baddest 47 aliibuka kama Msanii Bora Wa Dancehall kwa mwaka huu na kisha siku chache baadae kuachia ngoma yake ya “Mauzauza” ambayo kwa sasa inafanya vizuri. 

Nyimbo Mpya Tanzania Wiki Hii

Akizungumza kwenye mahojiano hivi karibuni na kituo cha Clouds FM, Baddest 47 amefichua kuwa, tofauti na mwaka jana, kwenye msimu huu wa mwaka huu wa tuzo za Tanzania Music Awards hakukuwa na zawadi zozote kwa washindi na badala yake waliondoka mikono mitupu. 

Harmonize SINGLE AGAIN Yaandika Historia Mpya TikTok

“Mwaka jana kulikuwa na zawadi, kulikuwa na bima ya afya lakini kwa mwaka huu tangu tuchukue tuzo pale juu kulikuwa hamna maelekezo yoyote zaidi ya After Party. Yaani kulikuwa hamna maelekezo yoyote kwamba hii tuzo inaambatana na nini. Kulikuwa na message kama hiyo kwenye group kwamba hamna chochote kinaambatana na tuzo” alizungumza Baddest 47 kwenye mahojiano hayo. 

Leave your comment