Nyimbo Mpya Tanzania Wiki Hii


[Picha: Instagram]

Mwandishi-Charles Maganga 

DOWNLOAD LATEST BONGO MUSIC MP3

Wasanii kutoka Tanzania wameendelea kutoa dozi kali ya burudani kwa mashabiki wa muziki nchini humo na Afrika Mashariki kwa ujumla na hii kutokana na nyota kutoa nyimbo mpya zenye mahadhi tofauti tofauti kama Amapiano, Hip hop, Bongo Fleva na zaidi.

Download Vavayo feat. Marioo - Whozu

Kutoka kwa wasanii kama Zuchu, Rayvanny, Mbosso na wengineo hizi hapa ni ngoma mpya Tanzania wiki hii :

Nani - Zuchu

Malkia wa WCB, wiki hii ameachia mkwaju wake wa kuitwa “Nani” ambao ni wimbo wake wa tatu kwa mwaka huu wa 2023.

Humu ndani Zuchu anachezesha mashabiki wake mitindo tofauti tofauti huku akiwa anatumia vionjo kutoka kwenye nyimbo za watoto kufikisha ujumbe wake.Gwede Gwede - Rayvanny & Baddest 47

“Shughuli Ni Watu, Ni Watu Ndo Sisi” huo ni mmoja wa mstari unaopatikana kwenye mkwaju mpya wa Rayvanny akiwa na Baddest 47.

Kwenye ngoma hii, utapenda namna ambavyo Rayvanny na Baddest 47 wanapokezana mashahiri na kubwa kabisa video ya ngoma ambayo imeongozwa na Eris Mzava pia itakuvutia.Amepotea - Mbosso

Baada ya kutesa mwaka 2022 na EP yake ya “Khan” Mbosso amerudi tena na kibao kipya cha kuitwa “Amepotea”

Huu ni wimbo ambao Mbosso anaonesha ni jinsi gani alivyoikimbia familia yake na kwenda kuishi na mwanamke anayempenda
Peleka Gari - Chudy & Dulla Makabila


Moja ya vitu mujarab kuhusu “Peleka Gari” ni namna ambavyo Chudy na Dulla Makabila wameweza kuwasilisha ujumbe wao kwa ufundi mkubwa sana. Kwa sasa hii ndio ngoma ya Singeli inayofanya vizuri nchini Tanzania kwa wiki hii.Success - Walter Chilambo Ft Jux


Kama unatafuta wimbo ambao utakupa tumaini na faraja pindi ukiwa unapitia changamoto mbalimbali basi hii hapa ya kuitwa “Sucess” ya kwake Walter Chilambo na Jux ni kwa ajili. Mashahiri mazuri na muingiliano mzuri wa sauti umechagiza ngoma hii kuwa ya kipekee sana.Harmonize SINGLE AGAIN Yaandika Historia Mpya TikTok

Aslay Adokeza Ujio Wa Tamasha Lake

 

Leave your comment