Wasanii 5 Bongo Ambao Wanamiliki Biashara Nje ya Muziki

[Picha: YouTube]

Mwandishi: Charles Maganga

Pakua Ngoma Zake Nandy Bila Malipo Kwenye Mdundo

Kwa muda mrefu sasa wasanii kutokea Tanzania wamekuwa wakianzisha biashara tofauti tofauti ili kuweza kuongeza na kupanua uwezo wao wa kiuchumi.

Free Download: Pakua mixes 7 Kali za Clouds FM ndani ya Mdundo

Tofauti kabisa na wasanii wa zamani, wasanii wa kizazi kipya wamekuwa wakitumia fedha ambazo wamezipata kupitia muziki na kuwekeza kwenye maeneo mengine ya biashara kama kuuza chakula, kufungua saluni, kuanzisha vyombo vya habari na sekta nyingine nyingi.

Wafuatao ni wasanii watano kutoka Tanzania ambao wameanzisha biashara au kampuni nje ya kufanya muziki :

Shilole

Kwa miaka sita sasa, Shilole amekuwa akitikisa sekta ya biashara ya chakula Tanzania kupitia mgahawa wake wa kuitwa "Shishi Food". Shilole ambaye ni msanii wa kike wa pili mwenye wafuasi wengi zaidi Instagram Tanzania amekuwa akitumia ushawishi wake mitandaoni kuvutia wateja wengi zaidi kwenye biashara yake. Biashara ya Shilole imekuwa ni mfano wa kuigwa nchini Tanzania na kufikia sasa ameweza kufungua matawi mawili ya mgahawa wa Shishi Food, wa kwanza upo Dar Es Salaam pamoja na jijini Dodoma.

Soma Pia: Mtasubiri ft Zuchu na Nyimbo Zingine za Diamond Platnumz Zilizofungiwa Tanzania

Rayvanny

Ukiachana na kuwa bosi wa lebo ya Next Level Music, Rayvanny pia ni mmiliki wa, mgahawa unaoitwa Havanna unaopatikana Mbezi Beach, Dar Es Salaam. Mara kwa mara amekuwa akitumia akaunti yake ya Instagram kutangaza mgahawa huo ambao unahusika kwenye kuuza chakula, vinywaji na pia ikiwa ni sehemu ambayo wapenzi wa soka hukutana kwa ajili ya kutazama mpira.

Bilnass

Bilnass ni mmiliki wa duka kubwa la simu na vya simu jijini Dar Es Salaam, la kuitwa Nenga Tronix na mara nyingi amekuwa akitumia akaunti yake ya Instagram kwa ajili ya kutangaza bidhaa mpya ambazo huingia dukani hapo. Mastaa tofauti tofauti kama mtangazaji wa Wasafi FM Baba Levo pamoja na msanii wa vichekesho Dull Vanny ni baadhi ya, wasanii wachache ambao washatemebela duka hilo.

Nandy

Ukiachana na kuuza vipodoi kama lipstick, Nandy anajulikana pia kwa umiliki wake wa saluni ya kupamba maarufu inayoitwa Nandy Bridal. Nandy Bridal hushughulika na kupamba maharusi wa jinsia ya kike na mara nyingi Nandy amekuwa akitangaza biashara yake hiyo kupitia akaunti yake ya Instagram.

Diamond Platnumz

Diamond Platnumz ukiweka kando kuwa mwanamuziki, Diamond Platnumz anamiliki biashara tofauti tofauti hasa katika tasnia ya burudani. Simba anamiliki Wasafi FM na Wasafi TV, kampuni ya kubeti ya kuitwa Wasafi BET, kampuni ya, kuzalisha na kutayarisha na kutengeneza video za muziki ya kuitwa Zoom Extra pamoja na Cheka Tu ambayo ni kampuni ya kutayarisha maonesho ya vichekesho na kusimamia wasanii wa vichekesho.

Leave your comment