Diamond ‘Ramadhan’, Tommy Flavour ‘Don’t Know You’ na Nyimbo Zingine Mpya Tanzania Wiki Hii

[Picha: Nyimbo Mpya]

Mwandishi: Charles Maganga

Pakua Ngoma Zake Nandy Bila Malipo Kwenye Mdundo

Ni wiki nyingine tena ambayo kiwanda cha muziki Tanzania kimepokea ngoma mpya kutoka kwa wasanii mbalimbali wa muziki ambazo zina lengo la kuburudisha na kuwafurahisha mashabiki. Zifuatazo ni ngoma tano mpya ambazo wasanii kutoka Tanzania wameachia ndani ya wiki hii:

Pakua Mixes Maalum Kwa Ajili Ya Mwezi Mtukufu wa Ramadan

Ramadhan - Diamond Platnumz 

 

Ili kuweza kuadhimisha vyema mwezi wa Ramadhan bosi wa lebo ya WCB Diamond Platnumz wiki hii ameachia ngoma mpya kabisa ya kuitwa Ramadhan ambayo amemshirikisha Mbosso pamoja na Ricardo Momo kutokea Wasafi. Hii ni ngoma ambayo ina lengo la kuhamasisha mfungo kipindi cha mwezi huu wa Ramadhan. Kupitia ngoma hii unaweza ukaburudika pamoja na kupata mawaidha mbalimbali kutoka kwenye mashahiri ya ngoma hii.

https://www.youtube.com/watch?v=8ikaEWBGElA

Don't You Know - Tommy Flavour 

Kutoka Kings Music mfalme wa RnB yaani Tommy Flavour aliweza kuchangamsha muziki wa Bongo Fleva baada ya kuachia ngoma yake mpya ya kuitwa Dont You Know. Don't You Know ni ngoma ya kwanza kwa Tommy Flavour kwa mwaka 2022. Kwenye mashahiri ya ngoma hii, Tommy Flavour anajaribu kumuaminisha mpenzi wake ni kwa namna gani anampenda sana.

https://www.youtube.com/watch?v=2H2sODEFEa0

Wamoto - Bright TZ Ft Mr Blue

Bright amerudi tena kwenye muziki na ngoma yake mpya kabisa ya kuitwa Wa Moto ambayo amemshirikisha Rapa Mr Blie. Wa Moto ni ngoma ambayo Bright na Mr Blue wanamwaga sifa za kutosha kwa binti mrembo kutokana na uzuri pamoja na urembo alionao. Mr Blue amepamba aya ya kwanza ya ngoma hii kwa mistari yake matata ya Hiphop kabla ya Bright kupamba kiitikio cha wimbo huu na sauti yake ya kubembeleza.

https://www.youtube.com/watch?v=z-svdFnoArk

Nimebadilishwa Jina - Angel Bernard

Mwanamuziki wa Injili kutoka Tanzania Angel Bernard wiki hii aliendeleza kusambaza habari njema baada ya kuachia wimbo wake unaoitwa "Nimebadilishwa Jina". Huu ni wimbo ambao Angel Bernard anashuhudia jinsi ambavyo maisha yake yamebadilika na kuinuliwa baada ya kumpokea Mwenyezi Mungu kwenye maisha yake ya kila siku. Bila shaka huu ni wimbo ambao unatoa faraja na tumaini kwa wale wote ambao huenda wanapitia changamoto tofauti tofauti.

https://www.youtube.com/watch?v=7g3y_L6dC1w

Ngosha - Young Killer Msodoki

Huitaji mda mwingi kufahamu kuwa ngoma mpya ya Young Killer Msodoki ya kuitwa Ngosha imeandikwa kwa ufundi mkubwa sana hasa upande wa mashahiri. Hii ni ngoma ambayo Young Killer anaonesha kujikubali na kuamini kwenye kipaji. Kikubwa hasa kwenye wimbo huu ni namna ambavyo Young Killer ameweza kucheza vizuri na maneno kwenye kibao hiki.

https://www.youtube.com/watch?v=bj55poH0OG4

Leave your comment