Ibraah ‘Rara’, Diamond ‘Mtasubiri’ ft Zuchu na Nyimbo Zingine Zinazotamba YouTube Tanzania Wiki Hii

[Picha: Mwananchi]

Mwandishi: Charles Maganga

Pakua Ngoma Zake Nandy Bila Malipo Kwenye Mdundo

Kama unapenda kusikiliza na kutazama video za muziki kutoka nchini Tanzania basi bila shaka utakuwa umeshatembelea mtandao wa YouTube ili kuweza kusikiliza na kurahani nyimbo mbalimbali kutoka kwa wasanii wa Tanzania. Kitu ambacho pengine wengi hawakijui ni kwamba mtandao wa YouTube kila baada ya muda hutoa orodha ya ngoma ambazo zinasikilizwa na kutazamwa sana kwenye mtandao huo mkubwa duniani na kwa upande wa Tanzania, orodha hiyo hutoa maana halisi ya msanii gani haswa anafanya vizuri sana. Zifuatazo ni ngoma 5 ambazo zinafanya vizuri sana YouTube Tanzania kwa wiki hii:

Free Download: Pakua mixes 7 Kali za Clouds FM ndani ya Mdundo

Mtasubiri - Diamond Platnumz ft Zuchu

Mtasubiri ya Diamond Platnumz na Zuchu imeendelea kufanya vizuri YouTube na pamoja na kwamba ina siku 9 tangu kuachiwa kwake lakini kufikia sasa imeshatazamwa mara 5.2. Ngoma hii pia iliweka historia ya kuwa ngoma ya kwanza barani Afrika kuwahi kufikisha watazamaji laki moja YouTube baada ya kufikisha idadi hiyo ya watazamaji ndani ya dakika 27 tu tangu kuachiwa kwake.

https://www.youtube.com/watch?v=IokCG2J-_5Q

Soma Pia: Diamond, Harmonize, Nandy na Wasanii Wengine Bongo Waliotoa Ngoma Kusifia Timu Zao Za Soka

Fine - Diamond Platnumz

Ngoma hii ya Fine inapatikana kwenye EP ya Diamond Platnumz ya kuitwa First Of All na pia ndio video ya kwanza kuachiwa kutoka kwenye EP hio ambayo ndani ya muda mfupi tangu kuachiwa kwake imeweza kupata mafanikio makubwa. Fine ni video ambayo ina kila hadhi ya kuitwa video ya kimataifa kutokana na ubora wa picha kuwa kiwango cha juu, stori nzuri pamoja na uhalisia wa Diamond Platnumz pamoja na wahusika wote wa kwenye video. Diamond Platnumz kupitia video ya Fine anakuwa msanii wa pili kutoka Tanzania kufanya video na Director TG Omori kutokea Nigeria baada ya Harmonize kufanya video ya Serious Love na Director huyo.

https://www.youtube.com/watch?v=QOGi0Qp_ciA

Siwezi - Nandy

Kama unapenda muziki mzuri basi huwezi kuacha kusikiliza ngoma ya ‘Siwezi’ ya kwake The African Princess yaani Nandy. Ngoma hii  imetayarishwa na Kimambo Beatz. Ngoma hii kwa sasa inafanya vizuri sana kwenye mitandao vya kijamii kutokana na ukweli kuwa mashahiri yake pamoja na video yamegusa hisia za watu wengi sana kiasi cha kupelekea mchekeshaji mahiri nchini Tanzania Stan Bakora kuweza kuitengenezea remix video ngoma hii. Kufikia sasa kibao hiki kimetazamwa mara Milioni 2.1 kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=FuK_yKDdmHo

Nawaza - Diamond Platnumz

Nawaza ni kati ya ngoma chache ambazo Diamond Platnumz amezungumzia maisha yake binafsi, marafiki, ndugu zake na hata hali ya mashabiki zake kiujumla siku akiondoka hapa duniani. Ngoma hii imepata mafanikio makubwa sana kwani wiki nne tangu kuachiwa kwake tayari imeshatazamwa mara Milioni 3.5 audio pekee kwenye mtandao wa YouTube. Ngoma nyingine ambazo Diamond Platnumz ameimba kuhusu maisha yake ni pamoja na ‘Utanipenda’ , ‘Nikifa Kesho’ pamoja na ‘Sikomi’.

https://www.youtube.com/watch?v=njxSViOtBbY

Rara - Ibraah

Rara ya Ibraah imezidi kutia fora kwenye mtandao wa YouTube kwani kufikia sasa imeshatazamwa mara Milioni 1.1 kwenye mtandao wa YouTube ikiwa ni siku 6 tu tangu kuachiwa kwake. Huu ni wimbo ambao Ibraah anafikisha ujumbe wa mapenzi kwa mwandani kwa kumpa sifa kedekede na kumhaidi kuwa atakuwa nae siku zote na wala hatamuacha. Hii ni ngoma ya kwanza ya Ibraah kwa mwaka 2022 baada ya kuachia Addiction aliyomshirikisha Harmonize Desemba mwaka 2021.

https://www.youtube.com/watch?v=mvu5un63InM

Leave your comment