Diamond, Harmonize, Nandy na Wasanii Wengine Bongo Waliotoa Ngoma Kusifia Timu Zao Za Soka

[Picha: Muungwana]

Mwandishi: Charles Maganga

Pakua Ngoma Zake Nandy Bila Malipo Kwenye Mdundo

Miaka ya hivi karibuni imekuwa ni jambo la kawaida sana kwa wanamuziki kutoka Tanzania kuonesha wazi wazi ni timu gani za soka kutoka Tanzania ambazo wao wanashabikia na kuzipenda. Wasanii hao wa Bongo Fleva hufanya hivyo kwa kushiriki kwenye shughuli mbalimbali za timu husika ikiwemo kwenda kuangalia mechi za mpira wa miguu hasa zikichezwa kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa.

Free Download: Pakua mixes 7 Kali za Clouds FM ndani ya Mdundo

Wasanii hao huenda mbali zaidi kwa kutunga nyimbo ambazo zina ladha tofauti tofauti kama Bongo Fleva, Amapiano na hata Singeli ili kuweza kuleta hamasa na amsha amsha kwa mashabiki wa timu husika ambazo mara nyingi timu hizo huwa ni Simba na Yanga. Wafuatao ni wasanii 5 kutoka Tanzania ambao kufikia sasa wameshatoa ngoma kwa ajili ya timu zao pendwa za soka :

Soma Pia: Matukio 5 Kubwa Yaliyopamba Tanzania Music Awards 2021

Diamond Platnumz

Diamond Platnumz kujiita Simba haikuwa ni kwa bahati mbaya kwani mwamba huyu wa Wasafi ni shabiki mkubwa wa Simba Sports Club yenye makao yake huko Msimbazi Dar Es Salaam. Kuonesha mapenzi aliyonayo kwa Wekundu hao wa Msimbazi, Diamond Platnumz aliachia ngoma yake ya kuitwa Simba Mwezi Agosti mwaka 2020 ambayo ilikuwa na mahadhi ya Singeli. Kufikia sasa, ngoma hio imeshatazamwa mara Milioni 2.1 kwenye mtandao wa YouTube. Hii ni ngoma ambayo pia Diamond Platnumz aliitumbuiza Agosti 23 kwenye tamasha la Simba Day Mwaka 2020 ikiwa ni ngoma ambayo iliweza kupagawisha sana mashabiki pale Uwanja Wa Benjamin Mkapa.

https://www.youtube.com/watch?v=OR2VPusQbwg

Harmonize

Taifa zima la Tanzania linafahamu kuwa Teacher Harmonize ni shabiki namba moja wa timu ya Yanga na hii ilishirihirishwa wazi Agosti 24 mwaka 2020 baada ya kuachia mkwaju wake wa kuitwa ‘Yanga’. Kwenye ngoma hiyo ya Yanga, Harmonize anapita kwenye mdundo wa singeli akiwa anaisifia timu hiyo kwa kucheza vizuri uwanjani huku akiwatania wapinzani wakuu wa timu hiyo yaani Simba. Harmonize aliweza kunogesha Tamasha la Yanga Day kwa kutumbuiza kwa ustadi mkubwa ngoma hii ambayo kufikia sasa imeshatazamwa mara Milioni 1.1 kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=G4erREVNWIY

Nandy

Agosti 26 Mwaka 2021, Nandy aliiaminisha Tanzania kuwa yeye ni mtoto wa jangwani baada ya kuachia ngoma yake ya kuitwa ‘Yanga’ ambayo ilisindikizwa na video ya muziki ambao ilinogesha zaidi kazi hiyo. Yanga ni ngoma ambayo mara zote husikika pindi tu timu ya Yanga inaposhinda na bila shaka huu ni wimbo ambao umependwa mno na mashabiki wengi wa timu ya Yanga. Hilo lilidhihirika kwenye tamasha la Yanga Day 2020 ambapo Nandy alitumbuiza ngoma hii mbele ya maelfu ya mashabiki.

https://www.youtube.com/watch?v=Zq4y7S6DfL8

Tunda Man

Ushabiki wake mkubwa kwa timu ya Simba umepelekea Tunda Man kuandika nyimbo takribani 5 kwa ajili ya klabu yake Simba na mara nyingi Tunda huonekana sehemu yoyote ambayo klabu ya Simba itakuwa na tamasha au mechi muhimu sana. Ngoma za Tunda Man ambazo ameimba kwa ajili ya klabu yake ya Simba ni pamoja na ‘Simba Tunajidai’, ‘Simba’, ‘Tamben’, ‘Kwa Mkapa Hatoki Mtu’ pamoja na ‘Wanakoroma’ ngoma ambayo amemshirikisha Abdu Kiba pamoja na Dulla Makabila.

https://www.youtube.com/watch?v=62QJaw8ShW8

Marioo

Baada ya Bia Tamu kufanya vizuri, Marioo hakuona hatari kufanya remix ya wimbo huo akiwa anaisifia klabu yake ya Yanga. Ndani ya muda mfupi tangu kuachiwa kwake, Yanga Tamu imepata mafanikio makubwa ikiwemo kutazamwa mara Milioni 1.1 kwenye mtandao ndani ya mwezi mmoja.

https://www.youtube.com/watch?v=ERkUsjhXS_k

Leave your comment