Vitu Muhimu Wasanii wa Bongo Wanafaa Kujua Kabla ya Kujiunga na Lebo za Muziki

[Picha: Hivisasa]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Ni ukweli kuwa huwezi kuongelea muziki wa Bongo bila kutaja lebo kubwa za muziki nchini humo kama WCB, King's Music na Konde Music Worldwide miongoni mwa nyingine. Pamoja na kwamba lebo hizo zina ushawishi mkubwa sana nchini humo, bado wasanii wengi wa Tanzania wanafanya kazi peke yao bila kuwa chini ya lebo.

Pakua Nyimbo za Ali Kiba Bila Malipo Kwenye Mdundo

Ni sawa kusema kuwa wasanii wengi wakubwa nchini Tanzania kama Diamond Platnumz, Rayvanny, Barnaba Classic, Zuchu, Harmonize, Ali Kiba, Darassa na hata Moni Centrozone kufanya kwao vizuri kumetegemea sana nguvu kubwa ambayo mameneja kama Sallam SK, Dorice Mziray na Babu Tale wa Wasafi, Jembe na Mjerumani wa Konde Gang na hata Aidan wa King's Music wameweka kuhakikisha wasanii wao wanafika mbali.

Pakua Nyimbo za Darassa Bila Malipo Kwenye Mdundo

Pamoja na kwamba kuna wasanii kama Marioo, Nandy, Jay Melody, Jux na hata Ben Pol ambao hawako kwenye lebo yoyote na bado wanazidi kuwika kwenye mbuga ya Bongo Fleva, ukweli ni kuwa bado pia wasanii wengi wanahitaji msaada wa lebo za muziki ili kung'arisha safari yao ya kimuziki.

Umuhimu wa lebo za muziki?

 Kusambaza kazi za msanii

Ni ngumu msanii kuanza kusambaza kazi zake mwenyewe kwenye mitandao ya kutiririsha muziki, redio, runinga na maDj mbalimbali. Ukiwa chini ya lebo, kazi hii inakuwa rahisi maradufu kama kuchovya chai kwenye mkate. Lebo ya WCB kwa mfano mwezi Aprili mwaka 2021 waliingia mkataba wenye thamani ya Tsh Bilioni 11 na kampuni ya Ziiki kwa ajili ya kampuni hiyo kusambaza kazi za wasanii wa lebo hiyo kama Diamond Platnumz, Rayvanny, Zuchu, Lavalava na Queen Darleen kwenye mitandao mbalimbali ya kuuza muziki duniani. Hii inamaanisha kwamba kazi za wasanii wa WCB sasa zinaweza kupatikana kwenye majukwaa tofauti tofauti ya kusambaza muziki duniani hata ile ambayo haipatikani Tanzania.

Lebo hukuza jina na hadhi ya msanii

Ndani ya miezi saba tu tangu kutambulishwa kwake mwezi Novemba mwaka 2020, Zuchu alishinda tuzo ya Afrimma kama msanii bora bora chipukizi ndani ya bara la Afrika. Hiki ni kitu ambacho kilikuwa hakijawahi kutokea tangu kuzaliwa kwa Tanzania. Hii ndio kazi ya lebo. Kumfanya msanii awe na thamani na kuheshimika kwa kazi nzuri anayoifanya. Wote tunakumbuka jinsi ambavyo Rayvanny alimpamba Mac Voice kipindi anatambulishwa. Rayvanny alimtafutia Mac Voice mahojiano (interview) na vituo vikubwa vya habari, alimkutanisha na wasanii wakubwa na ndio maana haikushangaza sana waandaaji wa tuzo za AEUSA walipomtaja Mac Voice kuwania kipengele cha msanii bora chipukizi barani Afrika kwa mwaka 2021.

Urahisi wa kupata collabo

Unakumbuka kipindi Ibraah ametia wino Konde Gang? Ibraah alikuwa ni msanii chipukizi kutokea kijiji cha Lukokoda huko mkoani Mtwara na mara tu baada ya kujiunga na Konde Gang mwaka 2020, Harmonize aliweza kumuunganisha Ibraah na wasanii wa Nigeria kama Skiibii kwenye ‘Subira’ pamoja na JoeBoy kwenye ‘Wawa’. Hatusemi Ibraah bila Konde Gang asingewahi kupata collabo na wasanii wa kimataifa, lakini kupitia Konde Gang, ilikuwa ni rahisi na iliweza kufanyika kwa urahisi zaidi kuliko angekuwa msanii anayefanya kazi peke yake. Hivyo basi kupitia lebo ya muziki, msanii ana uwezo wa kuchagua ni msanii gani anataka kufanya nae collabo.

Uwekezaji wa kutosha

Siku zote lebo kazi yake ni kuwekeza kwa msanii kwa maana ya kugharamia vitu kama video za muziki za msanii, mavazi atakayovaa, usafiri na collabo zake. Kuna lebo nyingine huenda mbali zaidi mpaka kununulia wasanii nyumba na magari. WCB bila shaka wako vizuri kwenye eneo hili kwani, kwa mujibu wa Diamond Platnumz, mwaka 2018 alitanabaisha kuwa kipindi anamtambulisha Harmonize alitumia takribani Milioni 115 kwa ajili ya kugharamia video za Harmonize ambazo ni ‘Aiyola’ iliyogharimu Tshs Milioni 39, ‘Bado’ iligharimu Milioni 51 na ‘Matatizo’ ambayo iligharimu Milioni 5.

Kuandaa matamasha ya msanii

Mara nyingi huwa ni changamoto sana kwa msanii kuandaa tamasha lake pekee yake ila ukiwa na lebo ambayo ina uwezo mkubwa wa kifedha, huwa ni rahisi sana kufanikisha hilo. Hata ukimuuliza Zuchu atakiri kuwa asingeweza kuandaa tamasha la ‘Zuchu Homecoming’, na ‘I am Zuchu’ bila msaada wa lebo yake ya Wasafi. Vivyo hivyo, kwa Ibraah lebo yake ya Konde Music Worldwide ilitoa mchango mkubwa sana kuandaa tamashal la ‘Ibraah Homecoming’. Kwa sasa, Harmonize anshughulikia tamasha lake la Afro East Carnival na Konde Worldwide iko kifua mbele kwenye maandalizi. Vile vile, tamasha za msanii Ali Kiba, Kings Music huchukua uongzi kataika maandalizi.

Changamoto zinazoweza kutokea ukijiunga na lebo za muziki

Licha ya kuwa lebo za muziki zina manufaa mengi kwa msanii, pia kuna changamoto zinoweza kutokea unapojiunga na lebo.

Wewe sio msanii huru tena

Baada ya kujiunga na lebo, wewe sio msanii huru tena. Hii inamaanisha kuwa huwezi toa ngoma bila kujadiliana na wasimamizi wako, huwezi fanya collabo na msanii yoyote yule, huwezi hudhuria tamasha bila kuidhinishwa na lebo na mambo mengine mengi. Hii changamoto kwa kuwa, iwapo uko kwenye lebo iliyo na wasanii wengi wakubwa, unaweza subiri kwa mda kabla ya kazi yako kuachiwa. Kwa mfano, ijapokuwa hii haijadhibitishwa rasmi, wasanii Chilly na Keed walisubiri karibu mwaka mmoja kabla ya kuachia kazi yao ya kwanza baada ya kujiunga na Konde Gang.

Kugawanya mapato

Unapojiunga na lebo, kitu cha kwanza unachofanya ni kutia saini kwenye mkataba wako na lebo huo.  Kwenye mkataba huo, moja kati ya vipengele vilivyo humo ndani ni jinsi ya kugawanya mapato. Kwa kuwa unajiunga na lebo ambayo intakupea meneja an watu wengine wa kukusaidia kwenya kazi yako, mapato yako yatapungua kwani, lebo hio itakuwa inakata asimilia fulani kabla ya kukupa masalio.  Hii ni changamoto hasa kwa wasanii wakubwa kwani wakitengeneza hela nyingi, lebo pia huchukua asilimia kubwa, hivyo kuwaacha wakihisi wamekandamizwa, ilhali hio ndio makubaliano kwenye mkataba walioweka sahihi mwanzoni.

Leave your comment