Nyimbo Mpya: Harmonize Aachia Ngoma Mpya ‘Mwaka Wangu’

[Picha: The Citizen]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki mashuhuri kutokea nchini Tanzania Harmonize ameachia ngoma yake mpya kabisa ya kuitwa ‘Mwaka Wangu’.

‘Mwaka Wangu’ ni ngoma ambayo Harmonize amelenga zaidi kwenye kutoa faraja kwa watu kwani kupitia ngoma hii Harmonize anaonesha namna ambavyo amepania kufanya mambo makubwa zaidi kwa mwaka huu.

Soma Pia: Sallam SK Afichua Jina la Msanii Aliyejiondoa WCB Hivi Karibuni

Harmonize pia anatoa ujumbe kwa maadui zake kuwa wajipange kwani amejipanga zaidi.

"Kwani wao waweze wana nini? Na mimi nishindwe nina nini? Nshachoka siku zote kuwa wa chini wengine wanakula kipupwe maofisini. Mlisema haolewi haolewi mbona kaolewa? Mlisema hapewi, hapewi mbona amepewa? Mwaka huu ni wangu, kutimiza ndoto zangu," anaimba Harmonize kwenye aya ya kwanza ya ngoma hii.

Soma Pia: Khadija Kopa Azungumzia Uhusiano Baina ya Diamond na Zuchu

Kimaudhui ngoma hii ni tofauti na ngoma mbili za mwisho za Harmonize yaani ‘Outside’ pamoja na ‘Serious Love’ ambazo mashahiri yake yalijikita kwenye mapenzi.

Mashairi ya ‘Mwaka wangu’ yamelenga kutoa hamasa zaidi na faraja kitu ambacho pia Harmonize alishawahi kukifanya kwenye ngoma yake ya ‘Never Give Up’ ya mwaka 2019 ‘Dunia’ ambayo ni ngoma nambari tisa kwenye albamu yake ya High School.

Ili kunogesha zaidi kazi hii, Harmonize ameachia video ya ngoma hii ambayo inamuonesha akiwa mtaani na watu wa kawaida tu wakiwa wanacheza na kuimba. Aidha, mitindo ya dansi iliyotumika kwenye video hii pia imefanya kazi hii kuwa ya kimataifa.

Video hii imeongozwa na Jabulant ambaye kwa muda mrefu sasa amekuwa ni mpiga picha na mtu ambaye amekuwa akizunguka na Harmonize kwenye matamasha tofauti ya kimuziki kuchukua video.

https://youtu.be/9Iu9eovU2V0

Leave your comment