Sallam SK Afichua Jina la Msanii Aliyejiondoa WCB Hivi Karibuni

[Picha: Wasafi Media]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Sallam SK ambaye ni meneja wa msanii Diamond Platnumz, hatimaye amefichua jina la msanii ambaye amejiondoa kwenye lebo ya WCB.

Hapo awali Mkubwa Fella, ambaye ni mmoja wa wasimamizi wa wasanii wa WCB, alidokeza kuwa kuna msanii mmoja ambaye yuko kwenye harakati ya kudonnoka kwenye lebo hiyo.

Soma Pia: Khadija Kopa Azungumzia Uhusiano Baina ya Diamond na Zuchu

Fella, hata hivyo, hakufichua jina la msanii huyo. Hii iliibua maswali mtandaoni huku mashabiki wakitaka kujua ni msanii mgani ambaye anaondoka WCB. Sallam SK kupitia mazungumzo kwenye mtandao wa Twitter alitoa jibu la swali hilo.

Kwanza kabisa, Sallam alieleza kuwa WCB iko na wanachama waliotambulishwa na wengine ambao bado hawajatambulishwa.

"WCB ina wasanii wapo waliotambulishwa na wasiotambulishwa, sidhani kaunguza picha," moja kati ya chapisho za Sallam kwenye mtandao wa Twitter ilsomeka.

SomaPia: Mkubwa Fella Athibitisha Msanii Mmoja Kuondoka Lebo ya WCB

Baada ya mazungumzo ya hapa na kule na mashabiki kwenye mtandao wa Twitter, Sallam hatimaye alikiri kuwa msanii anayeondoka WCB ni Hanstone. Kwa mujibu wa taarifa ya Sallam, Hanstone alikuwa mmoja wa wanachama wa WCB ambao hawakuwa wametambulishwa.

Ikumbukwe kuwa mwaka jana kulikuwa na vuta nikuvute kati ya Hanstone na lebo ya WCB. Kwa mujibu wa Babalevo ambaye ako na ukaribu na lebo ya WCB, Hanstone alikua na utofauti na usimamizi wa lebo hiyo. Hanstone, vile vile, kupitia ukurasa wake wa kijamii ameahidi mashabiki wake makubwa mwaka huu.

Leave your comment