Mkubwa Fella Athibitisha Msanii Mmoja Kuondoka Lebo ya WCB

[Picha: Ghafla]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Meneja wa mwanamuziki Diamond Platnumz Mkubwa Fella hivi karibuni amethibitisha kuwa tayari kuna msanii mmoja kutoka lebo ya WCB ameshajiondoa kwenye lebo hiyo.

Kupitia mahojiano aliyoyafanya hivi karibuni Meneja huyo alidokeza kuwa, hivi karibuni wakati anaongea na Diamond Platnumz, msanii huyo alithibitisha kuwa kuna msanii mmoja kutoka WCB anatarajiwa kujiondoa kwenye lebo hiyo kubwa barani Afrika.

Soma Pia: AY Azungumzia Muziki wa Amapiano Kupata Umaarufu Tanzania

"Mfano mdogo juzi nilimuuliza Naseeb Abdul bwana vipi na huyu anayeondoka kakudhulumu? Akaniambia Muziki bwana Bongo nishaijua, nikamwambia ndo inatakiwa hivyo," alizungumza Mkubwa Fella ambaye pia alihusika kuunda kundi la muziki la Ya Moto Band mwaka 2013.

Hata hivyo Mkubwa Fella hakutaja jina la msanii huyo ambaye ameshajiondoa kwenye lebo hiyo ambayo kufikia sasa inasimamia kazi za wasanii sita ambao ni Diamond Platnumz, Rayvanny, Zuchu, Mbosso, Lavalava pamoja na Queen Darleen.

Soma Pia: Diamond Platinumz Adokeza Ujio Mpya Wa Queen Darleen

Ikumbukwe kuwa tangu lebo hiyo ianzishwe mwaka 2015, kufikia sasa ni wasanii wawili tu ambao wameshaondoka kwenye lebo hiyo ambao ni Rich Mavoko ambaye aliondoka mwaka 2018 na mwaka mmoja baadae Harmonize pia alitangaza kuvunja mkataba na lebo hiyo na kuamua kuanzisha lebo yake ya Konde Music Worldwide.

Leave your comment