Diamond Platinumz Adokeza Ujio Mpya Wa Queen Darleen

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Bosi wa lebo ya WCB Diamond Platnumz hivi karibuni amedokeza kuhusu ujio mpya wa kimuziki wa msanii Queen Darleen ambaye pia ni mmoja wa wasanii wanaounda lebo ya WCB.

Simba alitoa taarifa hiyo kupitia akaunti yake ya Instagram uwanja wa Instastory baada ya kupakia picha ya Queen Darleen akiwa anarekodi ngoma studio na kuandika ujumbe kuwa "Y'all Not Ready For The Queen" akimaanisha bado mashabiki hawako tayari kumsikia Queen Darleen mpya.

Soma Pia: Marioo Ataja Sababu Ya Kuepuka Kufanya Collabo Za Kimataifa

Queen Darleen ambaye pia ana undugu na Diamond Platnumz amekuwa kimya kwa muda sasa bila kutoa ngoma yoyote kwani mara ya mwisho kutoa ngoma ilikuwa ni Machi mwaka 2020 alipotoa ngoma yake ya "Bachela" ambayo alimshirikisha Lavalava.

Kipindi cha ukimya wake Queen Darleen amekuwa akiunga mkono miradi tofauti tofauti ya wasanii wa WCB ikiwemo kuchaoisha ngoma mpya za wasanii wa WCB kwenye akaunti yake ya mitandao ya kijamii pamoja na kuhudhuria shughuli mbalimbali zinazoandaliwa na wasanii wa WCB.

Soma pia: Country Wizzy Akaribishwa Katika Lebo ya Roof Top Baada ya Kutoka Konde Gang

Queen Darleen alianza muziki mwanzoni mwa miaka ya 2000 na alipata umaarufu baada ya kushirikishwa kwenye ngoma za wasanii wakubwa kutokea Tanzania kama Dully Sykes na Inspekta Haroun ila wimbo wake "Wajua Nakupenda" aliofanya na Ali Kiba ndio ulimpatia umaarufu mkubwa.

Mwaka 2017 alijiunga na lebo ya WCBna tangu hapo ametoa ngoma tofauti tofauti chini ya lebo hiyo kama "Kijuso" aliyofanya na Rayvanny, "Mbali" aliyofanya na Harmonize pamoja na "Touch" ambao ni wimbo uliofanya vizuri kila kona ya nchi.

Leave your comment

Top stories

More News