Country Wizzy Akaribishwa Katika Lebo ya Roof Top Baada ya Kutoka Konde Gang

[Picha: Spotify]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Muda mfupi baada ya lebo ya Konde Music Worldwide kutangaza ukamilisho wa mkataba wake na msanii maarufu Country Wizzy, usimamizi wake wa zamani umemkaribisha kufanya kazi naye tena.

Kwa mujibu wa lebo ya Konde Music Worldwide, mkataba wa Country Wizzy ulikamilika rasmi mnamo tarehe 8, Januari 2022.

Soma Pia: Country Wizzy Akamilisha Mkataba Wake na Konde Music Worldwide

Petit Man, ambaye alikua mmoja kati ya mameneja wa Country Wizzy wakati alikua chini ya lebo ya Roof Top, amemkaribisha wafanye kazi pamoja. Kupitia ujumbe aliouchapisha mtandaoni, Petit Man alisema kuwa Country Wizzy aliaga usimamizi wake wa zamani ili kutafuta riziki zaidi, ila bado amekaribishwa nyumbani kwa sababu hakufukuzwa.

Petit Man vile vile alitoa shukrani kwa lebo ya Konde Music Worldwide na mashabiki kwa kumshika mkono nyota huyo.

"Ahsante sana familia ya @kondegang kwa kipindi chote mlichokuwa na @countrywizzy_tz na kufanya nae kazi nyingi pia nachukua nafasi hii kuwashukuru fans wote waliokuwa wakiendelea kusuport msanii mpk alipofika sasa hv," Petit Man aliandika mtandaoni.

Petit Man aliweka wazi kuwa Country Wizzy kuanzia sasa atakua chini ya usimamizi wa Dr. Xhexhe. "@big_xhexhe tumempokea @countrywizzy_tz kwa mara nyingine tena na milango ipo wazi na sikuwahi kuacha kumsupport sababu sisi familia welcome back ninja," ujumbe wa Peti Man ulisomeka.

Aidha, Country Wizzy amebaki kimya na hajadokeza lolote kuhusu usimamizi wake mpya.

Leave your comment