Country Wizzy Akamilisha Mkataba Wake na Konde Music Worldwide

[Picha: Citimuzik]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Lebo ya Konde Music Worldwide imetangaza kukamilika kwa mkataba wake na msanii maarufu Country Wizzy.

Kupitia chapisho liloliwekwa mtandaoni, Konde Music Worldwide iliwajulisha wafuasi wake kuwa mkataba huo ulikamilika mnamo tarehe nane, mwezi wa huu wa Januari.

Soma Pia: Harmonize Atangaza Kuachia Ngoma Mpya Hivi Karibuni

Ukamilisho wa mkataba huo ulifikiwa baada ya makubaliano baina ya upande wa Konde Music Worldwide na Country Wizzy.

Tangazo hilo linamaanisha kuwa Country Wizzy kwa sasa ni msanii huru anayejitegemea hadi atakaposainiwa na lebo nyingine.

Soma Pia: Producer Bonga Atangaza Kufanya Kazi na Konde Gang

Konde Music Worldwide ilimtakia heri Country Wizzy na vile vile kumshukuru kwa mchango wake katika lebo hiyo.

"Taarifa: Mkataba kati ya Konde Music Worldwide na @countrywizzy_tz umemalizika hii leo tar 8 January 2022. Kuanzia leo Country Wizzy atakuwa msanii anaejitegemea baada ya kufikia makubaliano ya pande zote mbili. Konde Music Worldwide inamtakia kila lenye kheri Country Wizzy kwenye career yake ya music pamoja na maisha kwa ujumla. All the best Wizzy," tangazo kutoka Konde Music Worldwide lilisomeka.

Kwa upande wake, Country Wizzy amebaki kimya kuhusu ukamilisho wa mkataba huo huku mashabiki wakisubiri kusikia kauli yake. Country Wizzy amekua mmoja kati ya wasanii tajika waliosaniwa kwenye lebo ya Konde Music Worldwide.

Alipokuwa kwenye lebo hiyo, Country Wizzy alitoa ngoma mbali mbali zilizofanya vyema mno. Kwa sasa mashabiki wanasubiri kujua ni mkondo upi muziki wa Country Wizzy utachukua.

Leave your comment