Harmonize Atangaza Kuachia Ngoma Mpya Hivi Karibuni

[Picha: Harmonize Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii nyota kutokea Tanzania Harmonize ametangaza kuwa ataachia wimbo mpya mwezi huu wa Januari. Harmonize aliweka wazi tangazo hilo kupita ukarasa wake wa Instagram.

Kwenye chapisho hilo, Harmonize alisema kuwa japo anafahamu kuwa mashabiki wake wanaburudika na albamu yake ya 'High School', atawaongezea ngoma moja ya kufungua mwaka.

Soma Pia:  Lebo Tano Kutoka Tanzania Zinazotarajiwa Kufanya Vizuri Mwaka 2022

 "Yes I know you are in the class #highschool but I got another sound to drop this January only one song please," chapisho la Harmonize mtandaoni lilisomeka.

Msanii huyo ambaye pia ni mkurugenzi mkuu wa lebo ya Konde Music Worldwide, hata hivyo, hakufichua habari zaidi kuhusu ngoma aliyokuwa akizungumzia.

Hapo awali Harmonize alidokeza ujio wa kazi kadhaa ikiwemo EP yake pamoja na msanii wa Kenya Otile Brown, kolabo baina yake na MB Dogg zikiwemo kazi nyingine. Hii itakua ngoma ya pili kutoka kwa Harmonize mwaka huu kwani tarehe mbili mwezi huu wa Janauari aliachia video ya ngoma ya tatu kwenye albamu ya 'High School' kwa jina la 'Serious Love'.

Soma Pia: Zuchu Adokeza Tarehe Atakayoachia Video Ya 'Kitu'

'Serious Love' ilipata mapokezi mazuri na kufikia sasa, takriban wiki moja baadaye, imetazamwa zaidi ya mara laki saba kwenye mtandao wa YouTube. Harmonize anaonekana kuuchukua mtindo wa kuachia ngoma mfululizo, jambo ambalo limemfanya kuzidisha mafanikio yake kimuziki.

Kwa sasa macho yote yako kwake Harmonize kuona kama ataendeleza mafanikio yake kwenye muziki kupitia ngoma hii inayotarajiwa.

Leave your comment