Lebo Tano Kutoka Tanzania Zinazotarajiwa Kufanya Vizuri Mwaka 2022

[Picha: Ghafla]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Biashara ya muziki nchini Tanzania imezidi kunawiri na hii ni kutokana na uwepo wa lebo mbalimbali ambazo zimezidi kustawisha kiwanda cha Bongo Fleva kwa kusimamia wasanii, kuwaandalia matamasha mbalimbali, kuwatafutia collabo za kimataifa pamoja na kusambaza kazi za wasanii kwenye mitandao ya kutiririsha muziki.

Soma Pia: Wasanii 5 wa Bongo Wanaotarajiwa Kuachia Albamu Mwaka 2022

Kutoka nchini Tanzania zifuatazo ni lebo tano za muziki ambazo zinatarajiwa kufanya vizuri zaidi kwa mwaka 2022:

Soma Pia: Wasanii Kutoka Tanzania Wanaotazamwa Zaidi Kwa Mwaka 2022

Next Level Music

Kwa sasa lebo hii ina wasanii wawili pekee ambao ni Rayvanny na Mac Voice ambaye ndani ya muda mfupi alipata mafanikio makubwa ikiwemo kutajwa kuwania kwenye tuzo kubwa za AEUSA zilizofanyika huko nchini Marekani. Kwa mwaka 2022, wengi wanategemea kuona wasanii wengi zaidi wanatambulishwa kwenye lebo hii kubwa hapa nchini Tanzania.

Wasafi Classic Baby (WCB)

Kwa mwaka 2021 lebo hii imefanya maajabu makubwa ikiwemo kutoa albamu ya Mbosso ya ‘Definition of Love’ pamoja na ‘Sounds From Africa’ ya Rayvanny. Mwaka 2022 bila shaka mashabiki hawana budi kujifunga mikanda kwani Diamond Platnumz anatarajiwa kuachia albamu yake ambayo inatarajiwa kuwa na ngoma 12 kali huku Zuchu nae wengi wakiwa wanashuku huenda akaachia albamu yake ya kwanza mwaka huu.

Kings Music

Lebo ya Kings Music iliweka rekodi mwaka jana baada ya kuachia albamu yake ya kwanza ya ‘Only One King’ pamoja na EP ya K2ga ya ‘Safari’. Kwa mwaka huu wa 2022, mambo yanatarajiwa kuwa sukari zaidi kwani Tommy Flavor ametangaza kuachia albamu yake ‘Heir To The Throne’ huku Alikiba nae siku chache zilizopita alitangaza kuleta albamu yake ya nne.

Konde Music Worldwide

Kupitia lebo hii kwa mwaka 2022 wengi wanategemea kuona albamu ya Ibraah, Cheed na Killy zikiingia sokoni huku kwa upande wa Anjella yeye anatarajiwa kuachia EP yake ambayo ilitakiwa kuingia sokoni mwezi Desemba lakini iliahirishwa. Bila shaka kutoka kwa Harmonize huu ni mwaka ambao tutaona video nyingi zaidi za muziki kutoka kwenye albamu yake ya ‘High School’.

High Table Sounds

Hii ni lebo ambayo inamilikiwa na Barnaba na inasifika kwa muziki mzuri hasa ule wenye mahadhi ya Bongo Fleva. Kikubwa kwa mwaka huu ni kuwa msanii mwingine wa lebo hiyo Ziddy Value anatarajiwa kufanya vizuri zaidi kwa 2022 kama alivyofanya mwaka jana kupitia EP yake ya ‘From The Street EP’.

Leave your comment