Wasanii 5 wa Bongo Wanaotarajiwa Kuachia Albamu Mwaka 2022

[Picha: K24 TV]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Ni sahihi kusema kuwa kama kuna kitu kilichokuza, kusherehesha na kupamba mwaka 2021 basi ni hulka ya wasanii tofauti tofauti kutokea Tanzania kuachia albamu na EP kali ambazo pasi na shaka  ziliburudisha mashabiki.

Kwa mwaka 2022 mambo yanatarajiwa kuwa sukari zaidi kwani nyota mbalimbali kutokea Tanzania wanatarajia kuachia albamu, wafuatao ni wasanii kutoka Tanzania wanaotarajiwa kuachia albamu ndani ya mwaka huu:

Soma Pia: Amapiano Tano Kutoka Tanzania Zilizofanya Vizuri Zaidi Mwaka 2021

Diamond Platnumz

Siku chache zilizopita kupitia akaunti yake ya Instagram, Diamond Platnumz alithibitisha kuwa ana nyimbo 51 ambazo ziko tayari kwa ajili ya albamu yake na kati ya hizo ni nyimbo 12 tu ndo inabidi ziwepo kwenye albamu yake mpya ambayo imekuwa ikiwa ikitayarishwa kwa muda mrefu sasa.

Alikiba

Baada ya kuachia ‘Only One King’, ni wazi kuwa Alikiba hayuko tayari kuchukua likizo kwani kupitia akaunti yake ya Twitter siku chache zilizopita, msanii huyo alidokeza kuwa huenda akaachia albamu mwaka 2022 baada ya kuandika "Thinking of releasing another album in 2022" kitu ambacho kilikosha mashabiki.

Soma Pia: Nyimbo Tano Kutoka Tanzania Zilizozua Utata Mwaka wa 2021

Tommy Flavor

Nyota huyu kutoka Kings Music kupitia mahojiano aliyoyafanya na mtangazaji Lil Ommy mwezi Oktoba mwaka 2021, alithibitisha kuwa yuko mbioni kuachia albamu yake ya kwanza aliyoipa jina la ‘Heir To The Throne’ ambayo huenda ikaingia sokoni mwaka 2022.

Ibraah

Akiwa kwenye ziara yake nchini Marekani mwishoni mwa mwaka jana, Ibraah alienda mubashara kupitia Instagram na kutangaza kuwa albamu yake iko tayari  na kutokea hapo amekuwa akitoa vionjo vya nyimbo zilizomo kwenye albamu hiyo.

Soma Pia:Nyimbo Tano Kutoka Tanzania Zilizozua Utata Mwaka wa 2021

Rosa Ree

Pengine ndiyo albamu ya Hip-hop ambayo inasubiriwa sana kwa mwaka 2022. Rosa Ree mara kadhaa amekuwa akidokeza kuhusu ujio wa albamu hiyo ambayo wasanii kama Frida Amani na Chemical wamethibitishwa kushiriki kitu ambacho kimezidi kuleta hari baina ya mashabiki wa muziki.

Marioo

Kama wewe ni shabiki wa Marioo basi weka tabasamu usoni kwani pengine mpishi huyo wa ‘Beer Tamu’ ataachia albamu yake ya kwanza  tangu aanze muziki, albamu ambayo kwa mujibu wa Marioo ilitakiwa iingie sokoni Septemba 25 mwaka 2021 lakini ilihairishwa.

Leave your comment

Top stories

More News