Amapiano Tano Kutoka Tanzania Zilizofanya Vizuri Zaidi Mwaka 2021

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Pamoja na kwamba chimbuko lake ni Afrika Kusini, mwaka 2021 wasanii mbalimbali wa hapa nchini waliotesha mizizi ya muziki wa Amapiano hapa Tanzania kutokana na kuachia ngoma za Amapiano ambazo zimefanya vizuri sana. Zifuatazo ni ngoma tano za Amapiano kutoka Tanzania ambazo zimefanya vizuri sana kwa mwaka 2021:

Soma Pia: Nyimbo Tano Zilizofanya Vizuri TikTok Kwa Mwaka 2021

Beer Tamu - Marioo

Kupitia ngoma hii, Marioo amezidi kuimarisha ufalme wake kwenye muziki wa Amapiano nchini Tanzania kwani ngoma hii ilisikika kwenye klabu na sehemu nyingi za starehe. ‘Beer Tamu’ ilichagiza wasanii wengine kutokea Tanzania kuachia ngoma ambazo ujumbe wake unasifia pombe ikiwemo ‘Addiction’ ya kwake Ibraah au ‘Acha Wanywe Pombe’ ya Rosa Ree.

https://www.youtube.com/watch?v=J5Ka53RZUtE

Teacher - Harmonize

Mara tu baada ya kudokeza wimbo huu kupitia akaunti yake ya Instagra, ‘Teacher’ ya Harmonize tayari ulikuwa ni wimbo pendwa baina ya mashabiki. Ubunifu wa Harmonize katika kutupa vijembe kwa washindani wake kwenye mistari ya wimbo huu pamoja na mitindo bora ya dansi iliyotumika kwenye video hii ni kitu cha kupigiwa makofi.

https://www.youtube.com/watch?v=mPVoKSc6LJo

Soma Pia: Nyimbo Tano Kutoka Tanzania Zilizozua Utata Mwaka wa 2021

Iyo - Diamond Platnumz

Kwa sasa ‘Iyo’ imeweka rekodi ya ngoma ya Amapiano kutoka Tanzania ambayo inetazamwa zaidi kwenye mtandao wa Youtube ikiwa imeshatazamwa mara Milioni 16. Hii ni ngoma ambayo Diamond Platnumz amethibitisha kuwa anaweza kuimba aina tofauti tofauti ya muziki ikiwemo Amapiano.

https://www.youtube.com/watch?v=UcOSSs3CNQ0

Chawa - Whozu, Rayvanny & Ntosh Gazi

Huu ni wimbo ambao una mashahiri mepesi huku ikiwa imeundwa na mdundo wenye nguvu kutoka kwa S2kizzy ikiwa na lengo la kutikisa zaidi kwenye klabu na sehemu tofauti tofauti na starehe. Kufikia sasa, ngoma hii imeshatazamwa mara Milioni 3.3 kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=OdeLCyEJLuU

Addiction - Ibraah ft Harmonize

Kama upo klabu au sehemu yoyote ya starehe na unatafuta ngoma ambayo itaendana na mazingira ya aina hiyo, basi ‘Addiction’ ya Ibraah ambayo amemshirikisha Harmonize ni ngoma ambayo itakidhi hitaji hilo. Ndani ya muda mfupi tu, ‘Addiction’ imekuwa ngoma kubwa sana na kufikia sasa imeshatazamwa mara laki tatu tisini na moja kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=aDH9It7oD-A

Leave your comment

Top stories

More News