Nyimbo Tano Zilizofanya Vizuri TikTok Kwa Mwaka 2021
22 December 2021
[Picha: YouTube]
Mwandishi: Charles Maganga
Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram
Ukweli ni kwamba TikTok ni mojawapo kati ya mitandao ya kijamii ambayo ina watumiaji wengi sana hapa nchini Tanzania na mara nyingi watumiaji wa mtandao huu hutumia nyimbo za wasanii mbalimbali pindi wanapojirekodi video. Zifuatazo ni ngoma tano kali kutoka Tanzania ambazo zimefanya vizuri zaidi Tiktok kwa mwaka 2021.
Soma Pia: Bifu Tano Kubwa Kwenye Bongo Fleva Mwaka 2021
Naanzaje - Diamond Platnumz
Huenda ikawa ndio ngoma iliyofanya vizuri zaidi kwa Afrika Mashariki kwenye upande wa Tiktok. Kufikia sasa, hashtag ya wimbo huu kwenye Tiktok imeshatazamwa mara Milioni 45 kwenye mtandao huo. Hii imechagizwa hasa na mashahiri mazuri yaliyopamba ngoma hii.
Sukari - Zuchu
Mashahiri yake mepesi ambayo watu wengi wa jinsia ya kike walikuwa wanaweza kuyaimba kwa urahisi ni kitu ambacho kimefanya ‘Sukari’ kuwa ni wimbo bora sana kwa watumiaji wa Tiktok kwa mwaka 2021. ‘Sukari Challenge’ ambayo ni hashtag iliyoanzishwa na Zuchu kufikia sasa imeshatazamwa mara Milioni 22.5 kwenye mtandao wa Tiktok
Soma Pia: Nyimbo Tano Kutoka Tanzania Zilizozua Utata Mwaka wa 2021
Kubali - Lody Music
Tangu ulipoachiwa Septemba 4 mwaka huu, ‘Kubali’ ya Lody Music ni ngoma ambayo ilipokelewa kwa mikono miwili na watumiaji wa Tiktok. Hii ni kutokana na ujumbe na mashahiri ya ngoma hii kuwa ya kugusa moyo hasa kwa, wale watu ambao wameumizwa na mapenzi.
Huba Hulu - Jay Melody
Mdundo mkali kutoka kwa Genius Jini pamoja na uandishi mzuri kutoka kwa Jay Melody ilipelekea mashabiki wengi hasa kutokea Tanzania na, Kenya kuupenda wimbo huo na kwenye mtandao wa Tiktok. Kufikia sasa, hashtag ya Huba Hulu kwenye mtandao huo imeshatazamwa mara Milioni 5.5.
Beer Tamu - Marioo
Huitaji kuwa na mahaba na pombe ili uweze kurahani ngoma hii ambayo kutokana na mdundo wake kuwa wa kuvutia watu wengi wanaotumia Tiktok walipenda kutumia ngoma hii kwenye video zao.
Leave your comment