Nyimbo Tano Kutoka Tanzania Zilizozua Utata Mwaka wa 2021

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Kuna wakati msanii huamua kuandika na kutunga nyimbo ambazo huleta gumzo na hali ya sintofahamu kwenye jamii inayomzunguka. Mwaka 2021, wasanii wengi waliachia ngoma ambazo mashahiri yao yalifanya mashabiki na wadau wa muziki washangae na kuhoji maudhui yake:

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Nay wa Mitego Aachia Wimbo Mpya 'Hunijui'

Zifuatazo ni ngoma tano kali kutoka Tanzania ambazo zilizua utata na kusababisha gumzo pale zilipoachiwa:

Soma Pia: Matamasha ya Muziki Tanzania Yaliyofanya Vizuri Zaidi Mwaka 2021

Nyamaza - Rayvanny

Kwenye ngoma hii ambayo iliingia sokoni mwezi Aprili, Rayvanny anatoa ushauri kwa aliyekuwa rafiki yake wa zamani kuwa anyamaze na kukaa kimya kuliko kuongea vitu ambavyo atakuja kuvijutia baadae.

Matumizi ya neno ‘Tembo’ na ‘Kaka wa Mtwara’ kwenye wimbo huu yalichagiza mashabiki na wadau wengi wa muziki  kuamini kuwa Rayvanny aliandika wimbo huu kwa ajili ya bosi wa Konde Gang yaani Harmonize, kitu ambacho kilipelekea mgogoro baina ya pande hizo mbili kuzidi kukolea.

https://www.youtube.com/watch?v=FRhxiyDhoyw

Baba - Nay Wa Mitego

‘Baba’ ni wimbo wa kisiasa ambao ndani yake Ney anamshtakia Hayati John Pombe Magufuli kuhusu madhila na matendo yanayotokea nchini Tanzania, tangu alipofariki mwezi Machi mwaka huu.  Huu ni wimbo ambao uliamsha hisia za watanzania kutokana na mashahiri yanayochoma moyo.

 https://www.youtube.com/watch?v=_11TVmqd4is

Hayakuhusu - Ibraah

Baada ya Rayvanny kuachia ‘Nyamaza’, siku hiyo hiyo saa chache baadae mwanamuziki Ibraah aliachia ngoma yake ya ‘Hayakuhusu’ ambayo wengi waliitafsiri kama diss track kwenda kwa upande wa pili.

https://www.youtube.com/watch?v=mzaaqiUXr8A

Weupe  - Mex Cortez

‘Weupe’ ni ngoma ambayo ndani yake rapa Mex Cortez anatema cheche kwa kikundi cha Hiphop cha Kikosi Kazi kuwa wajitathmini na wawaheshimu kundi la muziki la ‘Weusi’. Ngoma hii imepata mwitikio chanya kutoka kwa mashabiki na wadau wa muziki.

Mtaje - Harmonize

Kwenye ngoma hii Harmonize amemwimbia mrembo mmoja wa Bongo. Mashairi ya ngoma yanamsifia mrembo huyo ambaye Harmonize hajamtaja jina lake, lakini kulingana na vielelezo vya kimashahiri, wengi wameshuku huenda ngoma hiyo ni mahususi kwa Kajala Masanja ambaye alikuwa ni mpenzi wa zamani wa Harmonize.

https://www.youtube.com/watch?v=UbqLboruK8M

Leave your comment

Top stories

More News