Nyimbo Mpya: Nay wa Mitego Aachia Wimbo Mpya 'Hunijui'

[Picha: Nay wa Mitego Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii maarufu kutoka nchini Tanzania Nay Wa Mitego ameachia wimbo mpya kwa jina la 'Hunijui'.

Ngoma hii inazungumzia watu kueneza uvumi au kumzungumzia vibaya mhusika ambaye ni Nay Wa Mitego. Kama kuwajibu watu hao, Nay Wa Mitego kwenye ngoma hiyo anasema kuwa hao wanaomzungumzia vibaya hawamjui, na hivyo basi wamuache aishi maisha yake kwa furaha.

Soma Pia: Collabo 10 Kali Kutoka Tanzania Zilizofanya Vizuri Zaidi Mwaka 2021

Aidha, Nay Wa Mitego anasisitiza kuwa hababaishwi na maneno ya watu, na yeye ataendelea kuishi maisha yake.

"Ninachojua maneno hayavunjangi mifupa, wewe niseme na ukiishiwa maneno nitakupa, yaani ninavyoishi si kama wanavyotaka wao, wana habari zangu cha ajabu sinanga zao, hawanibabaishi hata waniwekee vikao, acha waongee maana mdomo mali yao, mimi, ukinichukia nami naitakuchukia, mimi, usipopiga nami sitokupigia, mimi, ukibeba goma langu nami nabeba la kwako pia, ukichepuka nami nachepuka pia dear," Nay Wa Mitego anaimba katika kipande cha ngoma hiyo.

Soma Pia: Diamond ‘Unachezaje’, Anjella ‘Toroka’ na Nyimbo Zingine Zilizoachiwa Tanzania Wiki Hii

Ngoma hii imetayarishwa na Mr T Touch ambaye ni moja ya watayarishaji wa muziki ambao wanaheshimika nchini Tanzania.

Video kwa upande mwingine imeelekezwa na Chiby Beat kwa ushirikiano na Gach B. Video ya wimbo huu imerokidiwa mjini Dar es Salaam.

Kilichowafurahisha mashabiki wengi kuhusu video ya wimbo huu ni jinsi Nay Wa Mitego amechukua uhusika ambao pia uko na uigizaji wa ucheshi.

Ngoma hii imepokelewa vyema na mashabiki na tayari ishatazamwa na maelfu ya mashabiki kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=7hxMHUqihd4

Leave your comment