Diamond ‘Unachezaje’, Anjella ‘Toroka’ na Nyimbo Zingine Zilizoachiwa Tanzania Wiki Hii

[Picha: Beka]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Tukiwa tunaelekea mwishoni kabisa mwa mwaka wasanii mbalimbali wameendelea kuachia ngoma tofauti tofauti ambazo zimezidi kusherehesha kipindi hiki cha mwaka ambacho watu wengi wako kwenye mapumziko. Zifuatazo ni ngoma tano mpya kutoka kwa wasanii wa nchini Tanzania ambazo zimetoka wiki hii.

Unachezaje - Diamond Platnumz

Mdundo mkali kutoka kwa S2kizzy umefanya ngoma hii ya ‘Unachezaje’ iwe bora sana na kupata watazamaji wengi YouTube ndani ya muda mfupi. Kufikia sasa video ya ngoma hii imeshatazamwa mara Milioni 1.8 kwenye mtandao huo.

https://www.youtube.com/watch?v=2x03Vz5x4t0

Soma Pia: Diamond ‘Unachezaje’, Harmonize ‘Utamu Remix’ na Ngoma Zingine Zinazotamba Bongo Wiki Hii

Toroka - Anjella ft Harmonize

Baada ya ngoma kama ‘Kama’ na ‘All Night’ kufanya vizuri, Anjella ameachia collabo yake ya tatu na Harmonize ya kuitwa ‘Toroka’. Ngoma hii ina mahadhi ya Amapiano na ndani yake Anjella na Harmonize wanasherekea na kuwahasa watu kufurahia maisha.

https://www.youtube.com/watch?v=y1T4doTSzA8

Vitamu - Platform ft Ruby

Baada ya ngoma yao ya ‘Katu’ kufanya vizuri, Platform pamoja na Ruby wamerudi tena na mkwaju wao mpya unaoitwa ‘Vitamu’. ‘Vitamu’ ni wimbo ambao ndani yake wasanii hawa wanasifiana kwa mahaba na mapenzi motomoto wanayopeana.

https://www.youtube.com/watch?v=89pc89uDR8M

Umeniteka - Christian Bella

Kama upo kwenye penzi zito na mwandani wako na unahisi kabisa umetekwa kihisia, basi wiki hii Christian Bella ametoa ngoma kwa ajili yako ya kuitwa ‘Umeniteka’. Hii ni ngoma ambayo inaashiria ujio mpya wa Christian Bella baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu kwenye muziki.

https://www.youtube.com/watch?v=AY7vVWgCCVs

Marry You - Barakah The Prince

Kwenye ngoma hii Barakah anakiri hisia alizonazo kwa mwanamke ampendaye huku akitumia maneno mazuri pamoja na kipaji chake cha sauti kutimiza hilo. Kufikia sasa, video ya ngoma hiyo ambayo imeongozwa na Adam Juma imeshatazamwa mara thelathini na moja elfu kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=URXBJgpitq8

Leave your comment