Diamond ‘Unachezaje’, Harmonize ‘Utamu Remix’ na Ngoma Zingine Zinazotamba Bongo Wiki Hii
16 December 2021
[Picha: Beka]
Mwandishi: Charles Maganga
Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram
Wiki ya pili ya mwezi Desemba ndio hii hapa imewadia na wasanii wa Tanzania wamezidi kuachia ngoma kali kupitia mtandao wa YouTube. Kati ya hizo, kuna baadhi zimeweza kupokelewa zaidi na mashabiki. Zifuatazo ni ngoma tano kutoka Tanzania ambazo zinafanya vizuri zaidi kwenye mtandao wa YouTube nchini Tanzania:
Soma Pia: Wasanii 10 Bora Tanzania Kwa Mwaka 2021
Unachezaje - Diamond Platnumz
‘Unachezaje’ ni ngoma ya tano ya Diamond Platnumz kwa mwaka huu. ‘Unachezaje’ imelenga kufurahisha, kuburudisha na kufanya watu waruke pindi wapo klabu na sehemu za starehe. Kufikia sasa, video ya ngoma hii imetazamwa mara laki sita sitini na nane kwenye mtandao wa YouTube.
Utamu Remix - Mabantu ft Harmonize
Baada ya toleo la kwanza la ngoma hii kufanya vizuri sana, bosi wa Konde Gang Harmonize aliamua kuongeza utamu kwenye ngoma hii ya ‘Utamu Remix’ ambayo mashahiri yake yanaburudisha, kuchekesha na kutoa mafunzo. Kufikia sasa, video ya ngoma hii imeshatazamwa mara laki nne thelathini na moja kwenye mtandao wa YouTube.
Paradiso - Stamina
Kwa wiki ya pili mfululizo, video ya ‘Paradiso’ imeendelea kufanya vizuri kwenye mtandao wa YouTube. Hii ni kutokana na ukweli kuwa video hiyo imepambwa na stori nzuri, uhalisia pamoja na ubora wa picha. Kufikia sasa, video hio imeshatazamwa mara laku tatu thelathini na mbili kwenye mtandao wa YouTube.
Ng'ari ng'ari – Lava lava
‘Ng'ari ng'ari’ imeendelea kung'ara katika mtandao wa YouTube kwa wiki hii. Hii ni kutokana na namna ambavyo Lava Lava anakuza na kutangaza ngoma kwenye mitandao yake ya kijamii. Kufikia sasa, ngoma hii imeshatazamwa mara laki sita ishirini na nane kwenye mtandao wa YouTube.
Weupe - Motra The Future
Kazi nzuri kabisa ya mtayarishaji wa muziki Mr T Touch imeendelea kufanya vizuri kwenye mtandao wa YouTube. Hii ni ngoma ambayo wengi wametafsiri kama ujumbe wa Motra The Future kwa kundi la Kikosi Kazi. Kufikia sasa, ngoma hii imeshatazamwa mara tisini na sita elfu kwenye mtandao wa YouTube.
Leave your comment