Nyimbo Mpya: ‘Sukari’ Zuchu, ‘Baikoko’ Mbosso na Video Zingine kutoka Bongo Zilizotazamwa Zaidi YouTube Mwaka wa 2021

[Picha: YouTube]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

2021 umekuwa ni mwaka mzuri kwa wasanii wa Bongo kwani wengi waliachia video kali kali. Kwenye nakala hii, tunaangazia video kali zilizifanya vyema YouTube Tanzania mwaka huu:

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Albamu na EP 10 Kali Zaidi Tanzania Kwa Mwaka 2021

Sukari - Zuchu

Tangu video hii ya ‘Sukari’ iachiwe mwezi Januari na msanii Zuchu, imeweza kufanya vizuri sana na kufikia sasa imeshatazamwa mara Milioni 60 kwenye mtandao wa YouTube. ‘Sukari’ imeweka  rekodi ya kuwa video ya muziki iliyotazamwa zaidi kwa mwaka 2021 sio tu nchini Tanzania, bali hata Afrika nzima.

Baikoko - Mbosso

Ubunifu pamoja na mitindo ya dansi iliyotumika, ndio imefanya video hii ya ‘Baikoko’ iliyoelekezwa na Director Kenny kuwa bora sana. Kufikia sasa, imeshatazamwa mara Milioni 29 kwenye mtandao wa YouTube.

Iyo - Diamond Platnumz

Mdundo huu wa Amapiano kutoka kwa Diamond Platnumz uliweza kupagawisha vilivyo mashabiki. Video ambayo imeongozwa na Hanscana kufikia sasa imeshatazamwa mara Milioni 16 kwenye mtandao wa YouTube. ‘Iyo’ ndio video ya Diamond Platnumz iliyofanya vizuri zaidi kwa mwaka 2021

Nyumba Ndogo - Zuchu

Ikiwa ni miezi mitano tu tangu kuachiwa kwake, video ya ‘Nyumba Ndogo’ imeshatazamwa mara Milioni 15 kwenye mtandao wa YouTube. ‘Nyumba Ndogo imeweka rekodi mpya ya kuwa ngoma ya singeli ambayo imetazamwa zaidi kwenye mtandao wa YouTube.

Naanzaje - Diamond Platnumz

Kama kuna video ya muziki ambayo Diamond Platnumz anaonekana akiiimba kwa hisia na kwa kumaanisha basi nii hii ya ‘Naanzaje’. Video hii kwa sasa imeshatazamwa mara Milioni 15 kwenye mtandao wa YouTube, ikiwa ni miezi mitatu tu imepita tangu kuachiwa kwake.

Soma Pia: Diamond, Nandy na Director Kenny Wang'aa Kwenye Tuzo Za Afrimma

Attitude - Harmonize

‘Attitude’ ni moja kati ya video za muziki zilizotikisa haswa kiwanda cha Bongo Fleva pale ilipovunja rekodi ya ‘Waah’ baada ya kutazamwa mara laki moja ndani ya dakika 44 tu. Kufikia sasa, video hii imeshatazamwa mara Milioni 14 kwenye mtandao wa YouTube ikiwa ndo video ya Harmonize iliofanya vizuri zaidi kwa mwaka 2021.

Kiuno - Rayvanny

Kufikia sasa kwenye mtandao wa YouTube, ‘Kiuno’ imeshatazamwa mara Milioni tisa. Kuanzia kwenye mandhari mpaka mavazi, Rayvanny aliamua kutuonesha ni kwa namna gani anajivunia uafrika wake . Hii ndio video ya Rayvanny iliyotazamwa zaidi YouTube kwa mwaka 2021.

Nimekuzoea - Nandy

Video ya ‘Nimekuzoea’ ilifanyika nchini Afrika ya Kusini kwa ushirikiano mkubwa na Em Pawa ya Mr Eazi. Hii ni video ambayo kufikia sasa imeshatazamwa mara Milioni 9 kwenye mtandao wa YouTube.

Jealous – Ali Kiba

Ilipofika Julai 30 mwaka huu, Ali Kiba aliamua kuwazawadia mashabiki zake video ya ‘Jealous’ ambayo bila shaka imebebwa na stori nzuri, vichekesho na ubora wa picha. Kufikia sasa, imeshatazamwa mara Milioni 8.9 kwenye mtandao wa YouTube

Mang'dakiwe Remix - Harmonize

Kutoka kwenye himaya ya Konde Gang, Harmonize kupitia ngoma ya ‘Mang'dakiwe Remix’ ambayo ilitoka mwezi Agosti imeweza kutazamwa mara Milioni 8.9 ndani ya miezi minne tu.

Leave your comment