Diamond, Nandy na Director Kenny Wang'aa Kwenye Tuzo Za Afrimma

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Tanzania iling'aa kwenye hafla ya tuzo za African Muzik Magazine Awards (Afrimma) ambayo ilifanyika tarehe 12 mwezi huu wa Disemba huko Marekani.

Bendera ya Tanzania ilipeperushwa kupitia wasanii watatu ambao ni Diamond Platnumz, Nandy na Director Kenny.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Lava Lava ‘Ng’ari Ng’ari’, Stamina ‘Paradiso’ na Ngoma Zingine Zinazovuma YouTube Tanzania Wiki Hii

Diamond Platnumz alishinda tuzo ya msanii bora wa kiume kutoka Afrika Mashariki kwa mwaka wa 2021. Nyota huyo aliwabwaga wasanii wenzake maarufu kwenye kitengo hicho kama vile; Eddy Kenzo kutoka Uganda, Ali Kiba kutoka Tanzania, The Ben kutoka Rwanda, Khaligraph Jones kutoka Kenya, Gildo Kassa kutoka Ethiopia, Otile Brown kutoka Kenya na Meddy kutoka Rwanda.

Diamond, vile vile, alishinda tuzo ya video bora ya mwaka kupitia wimbo wake wa ‘Berna’ ambao alishirikiana na Fally Ipupa na Mr Flavour.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Albamu na EP 10 Kali Zaidi Tanzania Kwa Mwaka 2021

Nandy kwa upande mwingine alishinda tuzo ya msanii bora wa kike kwa mwaka wa 2021. Nandy alikua katika kitengo kimoja na wasanii wengine kama; Zuchu kutoka Tanzania, Nadia Mukami kutoka Kenya, Vinka kutoka Uganda, Sheebah Karungi kutoka Uganda, Nikita Kering kutoka Kenya, Tanasha Donna kutoka Kenya na Knowles Butera kutoka Rwanda.

Director Kenny alishinda tuzo ya mwelekezaji bora wa video katika kitengo ambacho pia kilikua na TG Omori ambaye anafahamika kwa kuelekeza baadhi video bora za muziki barani Afrika.

Ushindi huu ulikua na maana kubwa kwa wasanii wa bongo baada yao kufanya vibaya kwenye tuzo za Afrima.

Leave your comment