Nyimbo Mpya: Lava Lava ‘Ng’ari Ng’ari’, Stamina ‘Paradiso’ na Ngoma Zingine Zinazovuma YouTube Tanzania Wiki Hii

[Picha: Biggest Kaka]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Imekuwa ni wiki ya aina yake kwenye kiwanda cha Bongo Fleva kwani nyimbo nyingi zimefanya vizuri kwenye mtandao wa YouTube, haswa zile ngoma za wasanii wa Hiphop. Zifuatazo ni ngoma tano za wasanii wa Tanzania ambazo zimefanya vizuri zaidi kwenye mtandao wa YoutTube:

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Albamu na EP 10 Kali Zaidi Tanzania Kwa Mwaka 2021

Weupe - Motra The Future

Rapa mwenye heshima yake kwenye muziki wa Hip-hop Motra The Future siku saba zilizopita aliachia mkwaju wake wa ‘Weupe’.Kutokana na mashahiri yake, wengi wameuchukulia kama diss track au wimbo uliolenga kuwasema kundi la Hip-hop la Kikosi Kazi.

https://www.youtube.com/watch?v=8cWj3qr3RtA

Ng'aring'ari – Lava lava

Ngoma ya ‘Ng'aring'ari’ kutoka kwake Lava lava imeendelea kufanya vizuri kwenye uwanja wa YouTube. Hii ni kutokana na mashairi ya ngoma hii kuwa ya kugusa sana hasa kwa wale watu ambao wameshawahi kuumizwa na mapenzi. Kufikia sasa, ngoma imeshatazamwa mara laki nne ishirini na nne kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=gK5KjpqRTDE

Amkia - Mex Cortez

Baada ya Motra The Future kutikisa Tanzania na ‘Weupe’, siku nne zilizopita rapa Mex Cortez aliachia ngoma ya ‘Amkia’ ambayo ndani yake Mex amemjibu rapa huyo kuwa ajitahidi kuheshimu kila msanii kwenye muziki kwani kila mtu ana nafasi yake.

https://www.youtube.com/watch?v=WaqrsqCcOBk

Paradiso - Stamina

Siku mbili zilizopita rapa Stamina aliachia ngoma yake ya ‘Paradiso’ ambayo pia imebeba jina la albamu. Kwenye ngoma hii ambayo imejaa vilio na majonzi, Stamina anaeleza kwa hisia mambo ambayo huenda yakatokea siku ya msiba wake. Kufikia sasa ngoma hii imeshatazamwa mara laki moja sitini na nane kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=1lLf4MOmDpw

Acha Niongee - Nay wa Mitego

Kama kawaida ya Nay Wa Mitego, kwenye ngoma hii ya ‘Acha Niongee’, Nay anagusia namna ambavyo watu wanamchukia kutokana na misimamo yake huku akiwahasa wasanii wenzake kutumia nafasi zao pia kuweza kuwasemea watanzania.

https://www.youtube.com/watch?v=pAqpA4ouOkY

Leave your comment