Collabo 10 Kali Kutoka Tanzania Zilizofanya Vizuri Zaidi Mwaka 2021
20 December 2021
[Picha: Beka]
Mwandishi: Charles Maganga
Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram
kufanya kazi na wasanii wengine aidha kutoka ndani au nje ya Tanzania ili kutengeneza kazi nzuri. Zifuatazo ni collabo kumi kali ambazo zimeachiwa na wasanii kutokea nchini Tanzania kwa mwaka huu:
Soma Pia: Wasanii 10 Bora Tanzania Kwa Mwaka 2021
Baikoko - Mbosso ft Diamond Platnumz
Hii ni moja kati ya collabo zilizotesa sana kwa mwaka 2021 na hii ni kutokana na ushirikiano mzuri ulioonekana baina ya Mbosso na Diamond Platnumz.
Ndombolo - Ali Kiba ft Abdu Kiba & Tommy Flavour
Hii ni ngoma ambayo inaonesha wazi ufundi na uwezo mkubwa walionao Kings Music kwenye suala zima la utunzi na uandishi wa muziki. Colabo hii iliwaleta pamoja wasanii wote walio chini ya Kings Music.
Ex Wangu Remix - Seneta Kilaka ft Hamisa Mobeto
‘Ex Wangu Remix’ ni moja kati ya ngoma za singeli ambazo zimepamba sana mwaka 2021. Hii imechagizwa na wazo zima la wimbo kuwa la kibunifu pamoja na ushirikiano mzuri wa kisanaa uliooneshwa kati ya Seneta Kilaka na Hamisa Mobetto.
Beer Tamu - Marioo ft Tyler ICU, Visca & Abbah Process
Huenda ikawa ndio ngoma ya Amapiano iliyotamba zaidi Bongo kwa mwaka 2021. Hii ni kutokana na namna ambavyo Marioo ameimba vizuri kwenye ngoma hii akitumia mdundo wenye nguvu ambao umetayarishwa na Abbah Process na Tyler Icu.
Kushki - Chege ft Saraphina
Ushirikiano mzuri kati ya Chege na Saraphina kwenye ‘Kushki’ umepelekea ngoma hii kuwa na uraibu wa kupitiliza hasa kwenye sehemu ya kiitikio ambacho mwanamuziki Chege ameweza kukitendea haki.
Lala - Rayvanny ft Jux
Wimbo huu uliweza kumkutanisha Rayvanny ambaye husifika kwa uwezo mkubwa wa kuimba pamoja na Jux ambaye wengi humsifu kwa sauti yake ambayo hutaradadi sana kwenye muziki wa RnB.
Unaua Vibe - Rapcha ft Young Lunya & Dwin
Moja kati ya collabo bora zaidi ya Hiphop kwa mwaka 2021. Hii ni kutokana na shauku ya mashabiki kuwa na hamu ya kumsikia Rapcha na Lunya kwenye ngoma moja. Baada ya ngoma hii kufanya vizuri hapa Tanzania, miezi minne baadae Rapcha aliachia ‘Unaua Vibe Remix’ akiwashirikisha Femi One na King Kaka kutokea Kenya.
For Your Love - Mbosso ft Zuchu
Hii ni ngoma ambayo imezidi kuthibitisha uwezo wa Mbosso kwenye uandishi wa nyimbo na uwezo alionao Zuchu kwenye kuimba pindi anaposhirikiana na Mbosso. Kupitia mitandao ya kijamii kama Tikitok, Instagram na Snapchat mashabiki wengi hasa wa kike wameonekana kuvutiwa sana na ngoma hii.
Iyo - Diamond Platnumz ft Focalistic, Mapara A Jazz & Ntosh Gazi
Kupitia collabo HII, Diamond Platnumz amezidi kudhihirisha anaweza kufanya kazi na msanii anayeimba aina yoyote ya muziki hapa barani Afrika.
Jealous - Ali Kiba ft Mayorkun
Kutoka kwenye albamu yake ya ‘Only One King’, ngoma ya Jealous haikufanya vizuri tu nchini Tanzania bali kila upande wa Afrika hasa ukitegemea kuwa ilikuwa ni moja kati ya ngoma chache ambazo Alikiba alishirikiana msanii kutokea nje ya Afrika Mashariki.
Leave your comment