Producer Bonga Atangaza Kufanya Kazi na Konde Gang

[Picha: Bongo 5]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwaka huu Producer Bonga amedhibisha kuwa mwaka huu atafanya kazi na lebo ya Konde Music Worldwide inayomilikiwa na msanii nyota Harmonize.

Producer Bonga na Harmonize wamekuwa na uhusiano wa kikazi kwa muda mrefu sana. Wawili hao walikua wakifanya kazi pamoja wakati Harmonize bado yupo WCB. Na hata alipoondoka WCB, Harmonize aliendelea kufanya kazi na Producer Bonga.

Soma Pia: Lebo Tano Kutoka Tanzania Zinazotarajiwa Kufanya Vizuri Mwaka 2022

Ila wawili hao walikumbana na tofauti ambazo zilimfanya Producer Bonga kusitisha uhusiano huo. Kwa mujibu wa Bonga, Harmonize hakua anakidhi matakwa na maslahi yake. Baada ya kuwa na tofauti hizo kwa muda, wawili hao wanaonekana wamesuluhisha mgogoro huo na hatimaye wapo tayari kufanya kazi pamoja tena.

Producer Bonga aliweka wazi taarifa hiyo kupitia ukurasa wake wa Instagram ambako shabiki alikuwa amemuuliza iwapo atafanya kazi na Harmonize mwaka huu. Mtayarishaji huyo wa muziki aidha aliongeza kuwa atafanya kazi na lebo ya Harmonize kwa makubaliano ya maandishi.

Tayari kuna kazi ambazo amehusika Bonga zipo njiani zaja mwaka huu, ashirio tosha kuwa Bonga amekuwepo Konde Gang kwa muda sasa, licha ya kudhibitisha uwepo wake saa hii.

Soma Pia: Babalevo Azungumzia Tetesi za Rayvanny Kuondoka WCB

Tangazo hili linatokea wakati ambapo Bonga vile vile ameingia kwenye tasnia ya muziki kama msanii. Kando na kusuka na kutayarisha midundo ya nyimbo, mwaka huu Bongo pia atatoa ngoma zake kibinafsi kama msanii.

Leave your comment