Exclusive DJ Mixes and 100% Ad-Free Music!
Babalevo Azungumzia Tetesi za Rayvanny Kuondoka WCB
6 January 2022

[Picha: Rayvanny Instagram]
Mwandishi: Brian Sikulu
Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram
Msanii maarufu kutoka Tanzania Babalevo ametoa kauli yake kuhusu tetesi za Rayvanny kuondoka lebo ya WCB. Tetesi hizo zimetamba mtandaoni haswaa baada ya Rayvanny kuanzisha lebo yake ya Next Level Music.
Maswali pia yameibuka kuhusu lebo ya WCB kutotambua mafanikio ya Rayvanny kimuziki kama vile hapo zamani.
Soma Pia: Nyimbo Mpya: Rayvanny Aachia Video Mpya Ya ‘Rara’
Babalevo ambaye pia ni mtangazaji wa Wasafi FM, na pia amejulikana kama msemaji wa lebo ya WCB, katika mahojiano ya hivi karibuni aliulizwa iwapo Rayvanny ameondoka lebo ya WCB.
Kwa mujibu wa Babalevo, Rayvanny kuondoka WCB sio jambo mbaya, bora iwe kwa amani na makubaliano.
Alieleza kuwa hakuna haja ya msanii kuwa katika lebo wakati anahisi amekua zaidi. Aliongeza kuwa iwapo Rayvanny hajajipanga kuwa msanii huru basi ni vyema asalie katika lebo ya WCB ili aendelee kupata manufaa ya lebo hiyo.
Soma Pia: Nyimbo Mpya: The Ben Aachia ‘Why’ Akimshirikisha Diamond Platinumz [Video]
"Mimi sioni kama ni kitu kibaya, kama Rayvanny ameona amefikia hatua ametosheka utaratibu upo nadhani watakuwa wamemuwekea yeye. Akitoka kwa amani na upendo sioni kama kuna ubaya wowote," Babalevo alisema.
Licha ya tetesi hizo kusheheni mtandaoni, Rayvanny bado anafanya kazi na lebo ya WCB kwa ushirikiano na lebo yake ya Next Level Music.
Katika kazi yake mpya ya 'Rara' kwa mfano, mtayarishaji wa muziki aliyehusika katika kuusuka mdundo huo ni Ayo Lizer kutoka WCB.
Weekly Top 10 songs

Trust No One3:13
chile-one-so-lucky4:02
Kamwambie3:47
Joy Is Coming3:08
Buwooma2:44
Udede Ft Msomali x Malume & Samas Alifata Hela Remix6:34
Msaliti 11:25
Leo3:39
Maringo4:00
NANI ft. Kamanda Pedeshee3:56
Top stories
- The Marathon
25 April
- Who Is Bad Beric
24 April
- Cashout by monyzoh boy
24 April
- MOSS Kay
24 April


Leave your comment