Nyimbo Mpya: The Ben Aachia ‘Why’ Akimshirikisha Diamond Platinumz [Video]

[Picha: YouTube]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii mashuhuri kutokea nchini Rwanda The Ben ameachia video ya wimbo wake mpya ‘Why’ ambao amemshirikisha nyota kutokea lebo ya WCB Diamond Platnumz.

Kabla ya video hiyo, ngoma ya ‘Why’ ilitangulia siku mbili zilizopita na kupata mafanikio makubwa kutokana na mashahiri yake kukaririka kwa urahisi na pia matumizi ya lugha tatu yaani kinyarwanda, kiingereza pamoja na Kiswahili.

Soma Pia: Wasanii Kutoka Tanzania Wanaotazamwa Zaidi Kwa Mwaka 2022

‘Why’ ni video ambayo inaonesha maisha ya wapenzi ambao wanapendana sana na kwa kuanza inamuonesha The Ben akiwa anakula raha na mpenzi wake ufukweni.

Baadaye Diamond Platnumz anaonekana akiwa kwenye sehemu iliyopambwa vizuri akiimba kwa hisia sana na mwisho kabisa The Ben na Diamond Platnumz wanaonekana tena ufukweni wakiendesha bodaboda na wenza wao.

Soma Pia: Wasanii 5 wa Bongo Wanaotarajiwa Kuachia Albamu Mwaka 2022

Kama kuna kitu kinachovutia kwenye video hii basi ni mtindo wa dansi ambao The Ben pamoja na Diamond Platnumz walikuwa wanaucheza kwenye kazi hii.

Hii ni video ambayo mandhari yaliyotumika ya ufukwe na bahari yamefanya video kuwa ya kuvutia sana kiasi cha kutukumbusha video ya ‘Despacito’ ya kwake Luis Fonsi pamoja na Daddy Yankee.

‘Why’ imeongozwa na nguli wa kuelekeza video za muziki kutokea nchini Rwanda aitwaye Irankunda Julien ambaye kwa sasa anatamba kwa kutengeneza video ya ‘Kamwe’ ambayo imeshirikisha wasanii tofauti tofauti kutokea Rwanda kama vile Bull Dog, Davis D, B Threy, Social Mula pamoja na B Threy.

 Kwa muda wa hivi karibuni, Diamond Platnumz amekuwa akishirikishwa kwenye ngoma za wasanii tofauti tofauti wa kimataifa kwani mwezi mmoja uliopita Diamond Platnumz alishiriki kwenye ngoma ya Serge Ibaka ya kuitwa ‘Tayari’ ambayo pia yupo Mohombi kutokea Congo.

https://www.youtube.com/watch?v=10tGnm2h9qQ

Leave your comment