Nyimbo Mpya: Rayvanny Aachia Video Mpya Ya ‘Rara’

[Picha: YouTube]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki mashuhuri kutokea nchini Tanzania Rayvanny hatimaye ameachia video ya ngoma yake pendwa ya kuitwa ‘Rara’.

‘Rara’ ni video ya kwanza kutoka kwa Rayvanny kwa mwaka 2022 na ni ngoma namba tano kutoka kwenye EP yake ya ‘New Chui’ ambayo aliiachia mwezi Oktoba mwaka 2021.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: The Ben Aachia ‘Why’ Akimshirikisha Diamond Platinumz [Video]

Kama mashahiri ya ‘Rara’ yalivyo, video ya ngoma hii pia imejawa na utulivu mkubwa na inamuonesha Rayvanny akiwa na mpenzi wake ufukweni wakiwa wanacheza na kufurahi.

Baadae wawili hao wanaonekana wakiwa kwenye chumba kilichojaa mapambo ya kutosha, Rayvanny akiwa anaimba huku mwanadada huyo mrembo akiwa anacheza.

Soma Pia: Wasanii 5 wa Bongo Wanaotarajiwa Kuachia Albamu Mwaka 2022

Kitu cha kuzingatia kwenye video hii ya ‘Rara’ ambayo imetumia wahusika wawili pekee ni kuwa kuna baadhi ya vipande huenda vikawa vinashabihana na ‘On The Low’ ya Burna Boy, ‘Jeje’ ya Diamond Platnumz au video ya ‘Essence’ ya kwake Wizkid pamoja na Tems.

Ubora wa picha, mavazi ya Rayvanny, mipangilio ya matukio na kikubwa mitindo ya dansi aliyoionesha mwanadada aliyepamba video hii ni mojawapo kati ya vitu ambavyo vimefanya video hii kuwa bora sana.

Eris Mzava ambaye ni mojawapo kati ya waelekezaji bora wa muziki nchini Tanzania ndiye ametayarisha video hii na kazi zingine za Rayvanny kama vile ‘Chawa’, ‘Sugu’ na nyinginezo nyingi.  

https://www.youtube.com/watch?v=qVo459zuKgo

Leave your comment