Marioo Ataja Sababu Ya Kuepuka Kufanya Collabo Za Kimataifa

Picha: Marioo Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki na mtunzi wa muziki kutokea Tanzania Marioo ameweka wazi sababu zinazopelekea yeye kuepuka kufanya ngoma na wasanii wa kimataifa kutokea nchi kama Nigeria pamoja na Afrika Kusini.

Akizungumza kupitia mahojiano aliyofanya na waandishi wa habari hivi karibuni Marioo alitanabaisha kuwa kwa sasa hayupo tayari kufanya collabo na wasanii wa mataifa ya nje kwani wengi wao hawaungi mkono kazi wanazofanya na watanzania pindi ngoma hizo wanazofabya pamoja zinapoingia sokoni.

Soma Pia: Marioo Afichua Mchango Wa Wizkid kwenye Tasnia Ya Muziki Nchini Nigeria

"Kihasara hasara tu hivi unafanya ngoma na mtu unadandia dandia mwisho wa siku unatoa ngoma ye anakausha tu, haposti au anaposti instastory haimake sense" alizungumza Marioo.

Marioo alizidi kudadavua kuwa collabo nyingi za kimataifa zinawanufaisha sana wasanii wa nje kuliko wasanii wa ndani ya Tanzania kwani hufanya wasanii wa nje kujulikana zaidi Tanzania kuliko wasanii wa Tanzania kujulikana zaidi kwenye mataifa ya nje.

Soma Pia: Fik Fameica, Harmonize ‘Champino’: New Music Uganda

"Nilichokigundua ni sisi ndo huwa tunawasaidia sana wao kuwaleta kwetu kuliko sisi kwenda kwao. Mwisho wa siku we utapromote ngoma huku utapromote itakuwa kubwa, labda alikuwa na uwezo wa kufabya show elements utampeleka akafanye show Dodoma, Arusha na sehemu nyingine ina maana na sisi pia tunaweza tukawa tunachangia kuwaleta huku" alizungumza Marioo.

Leave your comment