Marioo Afichua Mchango Wa Wizkid kwenye Tasnia Ya Muziki Nchini Nigeria
11 January 2022
[Picha: Marioo Instagram]
Mwandishi: Charles Maganga
Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram
Mwanamuziki mashuhuri kutokea nchini Tanzania Marioo hivi karibuni amefichua namna ambavyo msanii Wizkid ana mchango uliotukuka katika tasnia ya muziki ya huko nchini Nigeria.
Mfalme huyo wa Amapiano kwa hapa Afrika Mashariki, kupitia mahojiano aliyoyafanya hivi karibuni alizungumza kuwa Wizkid ni mojawapo ya wasanii wanaoheshimika sana Afrika kutokana na hulka yake ya kufanya ngoma na wasanii wadogo wanaochipukia.
Soma Pia: Nyimbo Mpya: Rapa Joh Makini Aachia Ngoma Mpya ‘Brand’
"Unajua wasanii wengi Afrika role model wao ni Wizkid. Kwa hiyo Wizkid vitu vingi anavyovifanya na watu ndo wanavifanya. Wizkid kafanya ngoma nyingi sana na vijana wa kwao mtu ana nyimbo moja, katoka au anaimba lakini anamchukua anapiga nae ngoma" alizungumza mtunzi wa Beer Tamu.
Marioo alizidi kudokeza kuwa Wizkid amekuwa akigharamia video za wasanii wachanga kutokea nchini Nigeria kitu ambacho kwa mujibu wa Marioo kinaanza kuigwa na wasanii tofauti tofauti kutokea nchini Tanzania. "Sometimes yeye (Wizkid) ndo huwaga anatoaga zile nyimbo yani nyimbo zake dogo anatia verse anampa, video nini anakaa anashoot unajua? Kwa hiyo watu wengi najua hiyo wataiiga kufanya, hivyo lakini sasa watachokosea wao wataiga kufanya, kazi na wasanii kutokea nchi tofauti " alizungumza Marioo.
Aidha Marioo alioneshwa kuchukizwa na baadhi ya wasanii wakubwa ambao wanawapa vipaumbele wasanii kutokea nchi za nje kuliko kufanya collabo na wasanii wachanga kutokea nchini Tanzania "Kwa sababu brothers wao wako tayari wafanye ngoma na underground kutokea Nigeria kuliko kufanya kazi na msanii ambaye anafanya vizuri hapa amekuja nini anaonesha kwamba kuna mahali anataka kwenda" alidokeza Marioo.
Leave your comment